Kamati kuwafuatilia wanaojifanya Machinga

DAR ES SALAAM :WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Selemani Jafo ameunda kamati ya watu 15 kwa ajili ya kufuatilia changamoto inayowakumba wafanyabiashara wa Kariakoo ya wawekezaji wageni wanaokuja nchini na ajenda ya ya uwekezaji kinyume chake wanajishughulisha na biashara za rejereja (Wamachinga) hivyo kuathiri uchumi wa wafanyabiashara wazawa.

Kamati hiyo itafanya kazi kwa siku 30 na itaanza kazi hivi karibuni ikiongozwa na Mwenyekiti wao Edda Tandi Lwoga Mkuu wa Chuo cha Elimu ya biashara ( CBE). Jafo amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na wafanyabiashara.

Jafo amesema timu hiyo itahakikisha kufanya utafiti kwa kina kwa soko la Kariakoo, kubaini ukubwa wa tazizo na wageni kufanya biashara nchini,kuchambua vibali na leseni zilizotewa na wageni na uhalali wake,kuchunguza sababu zilizochangia wageni kupewa vibali na leseni kwa kazi za biashara zinazostahili kufanywa na watanzani.

Aidha Jafo amesema kamati hiyo itafanya kazi ya kubaini sekta na aina ya biashara na maeneo yenye changamoto kwa wageni hapa nchini ,kuchunguza utaratibu na upatikanaji wa nyumba za wageni na biashara zao, kuchunguza udhaifu wa mfumo na uwezekano wa wageni kutumia njia zisizo rasmi kufanya biashara hapa nchini,hatua za haraka zitakazoweza kuchukuliwa na taasisi katika kudhibiti wageni wanaoingia kufanya biashara na ajira zinazostahili kufanywa na watanzania pamoja na kupendekeza mbinu za kuwezesha watanzania kupendekeza ushindani wao katika ajira ya kibiashara.

“Hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan amepokea kilio cha wanakariakoo na watanzania na hasa wafanyabiashara suala ambalo sasa hivi kumekuwa na mwingiliano wa wageni wengi ambao kubwa wanakuja na ajenda ya uwekezaji lakini kwa bahati mbaya uwekezaji wao hauakisi suala zima la uwekezaji wanapofika nchini changamoto zinazotokea ni kwamba wanashiriki katika shunghuli nyingine ambazo ni nje ya utaratibu za uwekezaji ambazo shughuli hizo hasahasa ni shughuli za kufanya biashara rejareja na kimachinga na mwisho wa siku huathiri mwenendo wa biashara kwa watanzania.

” Hii imekuwa kero kubwa kwa watanzania na wafanyabiashara na katoka hili kilio cha wafanyabiashara kimesikika na Rais Samia Suluhu Hassan ndugu zangu wafanyabiashara tanzania inaendeshwa kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni ambazo mgeni yeyote ambayo mtu yeyote anapaswa kufanya biashara kulingana na maelekezo ya serikali kumekuwa na wimbi la wageni ambao wakifanya biashara tofauti na utarati a wa kisheria na taratibu jambo hili limekuwa likileta kero kwa watanzania na hasa kwa vijana wetu na wafanyabiashara wazawa kiasi kwamba inaleta athari katika upande wa mitaji yao na mwisho wa siku tunatengeneza vijana ambao wamefilisika na kudaiwa na mabenki kwa wale waliochukua mikopo inaonekana wengene wanaanzisha magodouni na kuleta biashara hizo rejareja hivyo kuleta athari za kiuchumi ikiwemo kutokulipa kodi,” amesema jafo.

Aidha Jafo amesema sio kariakoo inaathirika bali hata na sekta nyingine kama sekta ya madini hivyo kamati hiyo itakuja na taarifa kamili ya nini kifanyike juu ya changamoto hiyo ili kusaidia nchi ni namna gani itanufaika pamoja na wafanyabiashara hao.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button