Ujenzi viwanja vya ndege umeleta historia

WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema ujenzi wa viwanja vya ndege vinne hapa nchi umejenga historia kubwa na matumaini yameonekana kuanza kukamilika kwake baadhi ya maeneo kwenye viwanja hivyo.

Profesa Mbarawa amesema hayo Februari 20,2025 katika ziara yake mkoani Shinyanga alipotembelea kiwanja cha ndege kilichopo kata ya Ibadakuli ambapo alieleza agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusu kutua kwa ndege nyakati ya usiku litafanyika.

Profesa Mbarawa amesema mikakati ya ununuaji wa vifaa vingine ufanyike kwa haraka na kufungwa kwani mkataba wa kukabidhi uwanja huo ni mwezi Aprili mwaka huu.

“Tunaweza kuanza kutumia kiwanja hiki kwa kuweka Mahema nje na kiwanja kuanza kufanya kazi kama ofisi wakati wa tukisubiri majengo mengine kukamilika,” amesema Profesa Mbarawa.

Profesa Mbarawa amewapongeza wakandarasi waliojenga uvumilivu wa kuhakikisha miradi ya ujenzi wa ndege katika viwanja vinne vya Sumbawanga,Tabora Kigoma na Shinyanga inakamilika na maeneo mengine kufikia asilimia 100.

Msimamizi wa ujenzi wa uwanja wa ndege kutoka Wakala ya Barabara Tanzania (Tanroads) mkoani Shinyanga Donatus Binamungu alisema Mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege kwa kiwango cha lami wenye urefu wa kilomita 2.2 ambapo kazi ya ujenzi ilianza rasmi mwezi April mwaka 2024 na Mkataba ulisainiwa Mwezi Juni mwaka 2017 kupitia Mkandarasi M/s China Henan International Cooperation Group Co.Ltd ( CHICO).

Binamungu amesema kazi zinazohusika kwenye mradi huo ni ujenzi wa njia ya kurukia ndege yenye urefu wa Mita 2200 na mita 30 ( runway) njia ya kuingilia na kutoka, Maegesho na kuhamisha miundombinu ya Maji,Umeme na Mawasiliano ambayo yote yanajengwa kwa kiwango cha lami na imekamilika kwa asilimia 100.

Mwakilisha wa Mtendaji Mkuu wa viwanja vya ndege nchini (TAA) Lugano Mwainuka amesema kiwanja cha Ndege kwa sasa kimefikia asilimia 94 kitakuwa ni kichocheo cha uchumi kitakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 120 na kuegesha Magari 160 kwa wakati mmoja zitatua ndege za ratiba na dharura zenye uwezo wa kubeba abiria 76.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha amesema wananchi wa mkoa huu walikuwa wakitegemea uwanja mdogo uliopo Kahama na wakati mwingine kulazimika kwenda Mwanza na eneo hili halina mgogoro wananchi wamelipwa fidia na mikakati ya uhamishaji makaburi unaendelea.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button