Wananchi Nanyamba kunufaika na mradi wa umwagiliaji

WANANCHI wa Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwara watanufaika na mradi wa umwagiliaji wa Arusha Chini kata ya Chawi utaogharimu zaidi ya Sh bilioni 14.

Akizungumza wakati wa mikutano ya hadhara, Mbunge wa Jimbo la Nanyamba, Abdallah Chikota amesema mradi huo ni mkubwa na wa kimkakati.

Mikutano hiyo imefanyika katika kijiji cha Navikole,  Ngonja, Arusha juu vilivyopo kata Chawi pamoja na kijiji cha Maembe chini kilichopo kata Kitaya.

Lengo la mikutano hiyo ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa viongozi hao kwenda kuzungumza na wananchi ili kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye maeneo yao na kuzifanyia kazi.

Pia kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali katika maeneo yao.

Aidha kupitia uwekezaji wa mradi huo, mbunge huyo amewataka  wananchi hao kuchangamkia fursa hiyo kwa kujikita katika kilimo cha umwagiliaji ili wawe na kilimo cha muda wote badala ya kutegemea mvua pekee.

Hata hivyo  mradi huo utawasaidia kufanya kilimo  kitachowasaidia kuwa na uchumi endelevu kwa kipindi cha mwaka mzima kama vile mboga mboga na kingine  badala ya kusubiri uchumi unaotokana na zao la korosho pekee.

“Huu mradi ni mkubwa kwahiyo tuchangamkie  tufanye kilimo mbadala wa zao la korosho ili tuweze kujipatia kipato endelevu,  fuchangakie hii fursa tukiacha watakuja watu kutoka maeneo mengine kuja kuchangamkia hii fursa” amesisitiza Chikota.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button