Chuo ISW chafundisha kozi malezi ya watoto

CHUO cha Ustawi wa Jamii(ISW) Kampasi ya Kisangara mkoani Kilimanjaro kimeonesha umuhimu na umahiri wa ufundishaji wa kozi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto.
Akizungumzia umuhimu wa utoaji mafunzo hayo katika maonesho yanayoendelea kwenye viwanja vya TBA mkoani Arusha, Meneja wa Chuo cha Ustawi Wa Jamii Kampasi ya Kisangara Mkoani Kilimanjaro, Dk, Leah Mwaisango amesisitiza baadhi ya vifaa vinavyotumika kufundishia katika darasa mfano la kozi hiyo vinaoneshwa kuwa ni kozi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto.

Amesema chuo kinatoa kozi ya ustawi wa jamii kuanzia ngazi ya cheti hadi shahada ya kwanza ikiwemo kozi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ngazi ya cheti na dilpoma kuanzia miaka name kushuka chini.
“Kozi ya malezi na makuzi ya mtoto inalenga kumsaidia mtoto katika masuala ya lishe,uchangamfu ambapo wanafunzi hufundishwa chuoni hapo hicho kinaandaa walezi na wasimamizi wa vituo vya kulea watoto ambao wanasimamia usalama wa mtoto, elimu ya awali, saikolojia ya mtoto, ubunifu, mbinu za malezi ya mtoto, afya na lishe na uchangamshi wa awali wa mtoto kupitia michezo.

Amesema kozi hiyo ya malezi na makuzi pia ni muhimu kwa walimu kufundisha wanatoto wa awali ambapo wanafunzi wanaosoma chuoni hapo wanatengeneza vitu mbalimbali vinavyowasaidia watoto kuhusu stadi za maisha, saikolojia ya mtoto pia wanaweza kutambua vipaji vyao na kuanza kutunzwa akiwa mdogo.
Amesisitiza watoto wanahitaji kuimbiwa kupigiwa malimba ikiwemo kujifunza na kutoa burudani sanjari na ufinyanzi unaomwezesha mtoto kujiajiri kwa kufanya kazi za mtoto kwani anayeandaliwa kumfundisha mtoto anafundisha jinsi ya kumwandaa mtoto kubuni mambo mbalimbali.




