Mbunge ahimiza wakulima wa korosho kujisajili

KUELEKEA msimu wa kilimo cha zao la korosho mwaka 2025/2026, wakulima wa zao hilo katika Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwara wamehimizwa kutoa ushirikiano kwa maofisa ugani kilimo waliopo kwenye maeneo yao kuhusu ukamilishaji wa usajilii wa wakulima hao.

Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Abdallah Chikota ametoa wito huo wakati wa mikutano mbalimbali ya hadhara iliyofanyika kwenye vijiji vya halmashauri ya mji Nanyamba.

Lengo la mikutano hiyo ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi zinazowakabili katika maeneo yao na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kwenye halmashauri hiyo ikiwemo ya maji, afya, elimu, barabara na umeme .

Miongoni mwa vijiji hivyo ni Misufini, Nachuma, Kiromba chini, Mikumbi, Kiromba, Mjimwema, Ngonja, Navikole Likwaya, Namtumbuka na majengo.

Amesema lengo usajili ni kuboresha taarifa au kanzidata za wakulima hao ili pembejeo za korosho au huduma yoyote itakayotolewa na serikali iwafikie wakulima husika ambapo awali kulijitokeza changamoto wakati wa utekelezaji.

‘’Kuna baadhi wa watu ambao walitumwa kufanya kazi hii ya usajili wa wakulima baadhi yao walileta taarifa zisizokuwa sahihi kwa hiyo unakuta pembejeo zinakwenda kwa watu ambao siyo wakulima lakini wakulima sahihi wasipate pembejeo,’’amesema Chikota.

Ameongeza: ‘’Unakuta watu wenye mashamba makubwa wanapata pembejeo chache lakini wale ambao wameandika mezani kwamba wana ekari hamsini, arobaini wanapata pembejeo nyingi na matokeo yake kuzua malalamiko katika jamii’.’

Aidha maofisa hao ugani walioko kwenye halmashauri hiyo pamoja na maeneo mengine yanayozalisha korosho nchini wameajiriwa na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) ili kuwezesha ufanisi wa zoezi hilo la usajiri wa wakulima.

Ajira hizo za maofisa ugani zilizotolewa na CBT ni utekelezaji wa Programu ya Jenga Kesho iliyo Bora katika zao la korosho (BBT) ambapo maofisa ugani wote walioajiriwa ni 500, waliyopelekwa halmashauri hiyo ni 25 kati ya 245 walipelekwa Mkoa wa Mtwara.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button