RC Mtwara ataka dua zaidi uchaguzi mkuu 2025

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala amewaomba viongozi wa dini mkoani humo kuendelea kuuombea mkoa huo na taifa kwa ujumla hasa wanapoelekea katika uchaguzi mkuu mwaka 2025.

Hayo yamejiri wakati wa ghafla fupi ya iftari iliyofanyija Manispaa ya Mtwara Mikindani na kuwakutanisha waumini wa dini zote wa mkoa huo iliyoandaliwa na ofisi ya mkuu wa mkoa huyo.

Amesema wakiwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani pamoja na kwarezma waendelee kuliombea taifa kwenye kipindi hicho cha uchaguzi ili ukawe uchugu wa amani.

“Tuendelee kuwaombea waumini wetu waende wakawachague viongozi wataowaongoza waliyosahihi na wenye kumcha Mungu na kumuogopa Mungu, twende tukawaambie waumini wetu kwamba wale viongozi wanaotaka kutugawa wasiwape nafasi,”amesema Sawala.

Hata hivyo amewashukuru viongozi hao wa dini kwa namna wanavyoendelea kuwaongoza kiroho, kimwili kwa kuwafundisha yaliyokuwa mema na kuchukia mabaya lakini kudumisha utulivu katika mkoa huo.

Pia kwa ushirikiano wao na serikali katika kutekeleza mambo mbalimbali yanayohusu waumini wao ambao ndiyo wananchi waliyopewa dhamana ya kushirikiana nao katika kuiongoza Mtwara.

Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Jamaldini Chamwi amewataka waumini ya dini zote mbili kuendeleza hali ya amani wakati wote ili kudumisha mshikamano waliyokuwa nao.

“Kwavile tupo ndani wa mwezi mtukufu wa Ramadhani niwaagize mahimamu wangu wa misikiti mbalimbali tutumie fursa hii kumwomba Mwenyezi Mungu atudumishie hali yetu hii ya amani na utulivu na upendo utawale ndani ya nchi yetu”amesema Chamwi

Meya wa Manispaa hiyo, Shadida Ndile amemshukuru mkuu huyo wa mkoa kwa moyo wake wa ushirikiano na wanamtwara wakati wote ikiwemo wa furaha na majanga huku akiwashukuru viongozi hao wa dini kwa kuendelea kumwombea Rais Samia Suluhu Hassan ili aweze kuimarisha afya yake pamoja na utendaji wake.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button