‘Afya ya kinywa hatari kifafa cha mimba, ulemavu’

MTWARA; KUTOKUTUNZA afya ya meno na kinywa ni moja ya sababu kwa wajawazito kupata watoto njiti, kifafa cha mimba, mimba kutoka na hata kupata watoto walemavu.

Mkurungezi Msaidizi wa Huduma za Tiba ya Meno na Kinywa kutoka Wizara ya Afya, Dk Baraka Nzobo, amesema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya ya Meno na Kinywa Kitaifa mkoani Mtwara juzi.

Amesema wajawazito wasipokuwa na uchunguzi wa mara kwa mara kuhakikisha afya imara ya meno na kinywa, wanapata madhara ambayo huathiri mimba.

“Magonjwa ya meno na kinywa yanazuilika pia yanatibika,” amesema huku akiwataka wajawazito na wazee kufanya uchunguzi wa mara kwa mara kulinda afya ya meno na kinywa.

Dk Nzobo amesema serikali imeimarisha huduma za tiba ya afya ya meno na kinywa katika hospital za rufaa, halmashauri na vituo vya afya vya kimkakati, huku akitaka wananchi hasa wajawazito na wazee kwenda kufanya uchunguzi wa mara kwa mara na kupata tiba inapohitajika.

Amesema serikali imetoa kiasi cha Sh bilioni 13 ndani ya miaka minne ambayo imesaidia kununua vifaa tiba maalumu vya afya ya kinywa na meno na kuimairisha huduma , kuajiri wataalamu wa afya ya meno na kinywa katika hospitali za rufaa za mikoa, halmashauri na vituo vya afya nchini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button