Vigogo Wachina watua kwa Ulega, wajitetea

HATIMAYE Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amekutana na viongozi wakuu wa kampuni za China zinazosimamia miradi ya ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (BRT), madaraja na barabara nchini kutafuta suluhisho la miradi inayosuasua kukamilika.

Mazungumzo ya Ulega na viongozi wa kampuni hizo yalifanyika katika Ofisi za Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Dar es Salaam jana na wamekubaliana kuhusu maendeleo ya miradi hiyo.

Ulega alisema mkutano huo ni mwendelezo wa hatua alizochukua baada ya ziara yake Machi 4, mwaka huu alipokagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya BRT4.

Wakati wa ziara hiyo wakandarasi waliokuwa katika eneo la mradi walishindwa kutoa majibu kuhusu ucheleweshaji wa kazi hivyo Ulega akaagiza viongozi wakuu wa kampuni hizo waitwe kutoka makao makuu yao nchini China.

“Tumepata nafasi ya kuzungumza nao. Wameeleza changamoto zao ingawa hazilingani na muda mwingi uliopotezwa. Hata hivyo tumeweka ahadi mpya za kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa,” alisema Ulega.

Katika kikao hicho kampuni ziliweka ahadi za kimaandishi kwa serikali kuhusu ukamilishaji wa miradi.

Miongoni mwa kampuni hizo ni Shandong inayotekeleza ujenzi wa miundombinu ya BRT kutoka Mwenge hadi Tegeta.

Nyingine ni China Geo Corporation (CGC) inayojenga barabara ya kutoka katikati ya jiji hadi Mwenge na Mwenge hadi Ubungo kupitia barabara ya Sam Nujoma.

Pia, Ulega alieeleza kukerwa na ucheleweshaji wa kampuni ya Shandong kwenye mradi wa barabara ya Omurushaka – Kyerwa.

Viongozi wa kampuni hiyo wamekiri tatizo hilo na waliahidi kuanza kazi mwishoni mwa Aprili, mwaka huu na Ulega amepanga kufanya ukaguzi mwanzoni mwa Mei, mwaka huu.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, mradi wa BRT4 unapaswa kukamilika ifikapo Aprili 30, mwaka huu lakini wakandarasi wameomba nyongeza ya muda wa miezi 12.

Serikali kupitia kwa Ulega imesema inachakata ombi hilo kwa kuzingatia njia mbili: kuvunja mikataba au kuongeza muda kwa masharti madhubuti.

Wakandarasi wametaja changamoto kadhaa zilizosababisha ucheleweshaji ikiwa ni pamoja na mvua za El Niño, ucheleweshaji wa kuhamishwa kwa nyaya za umeme, mabomba ya maji na gesi

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button