DUWASA yasaini mkataba wa bilioni 5 kutatua uhaba wa maji Dodoma

DODOMA: WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema Rais Samia Hassan ameelekeza utekelezaji wa miradi ya maji yenye thamani ya Sh bilioni 45 ambayo imelenga kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Maji Jijini Dodoma.

Miradi hiyo minne inatekelezwa ikilenga kuboresha huduma za maji kwa Jiji la Dodoma wakati ikisubiriwa utekelezaji wa miradi mikubwa ya maji ikiwa ni ile ya Mradi ya kuleta maji kutoka Ziwa Victoria na mradi wa Bwawa la Farkwa ambayo maadalizi ya utekelezaji inaendelea.

Akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji wa saini wa mkataba wa awamu ya pili ya Mradi wa Nzuguni kati ya Mamlaka ya Majisagi na Usafi wa Mazingira Dodoma(DUWASA) na Mkandarasi Bahaji Constraction wenye thamani ya Sh bilioni 5.6 unaotekelezwa kwa miezi 15 na umelenga katika kusambaza maji kutoka chanzo cha visima vya maji vya Nzuguni.

“Mbunge wenu (Anthony Mavunde) alileta maombi kwa Mheshimiwa Rais Samia juu ya uchimbwaji wa visima virefu aliposimama kusalimia wananchi pale Mpunguzi na sisi Wizara tukapata maelekezo ambayo tumeyafanyia kazi baada ya Rais kutoa fedha za kutekeleza hii miradi minne ambayo imelenga kuboresha huduma za majisafi katika Jiji la Dodoma wakati tunasubiri utekelezaji wa miradi ya Ziwa Victoria na ule wa Farkwa.”

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso

Aliitaja miradi hiyo mbali na ule wa usambazaji maji ya visima unaogharimu Sh bilioni 5.63 kuwa ni mradi wa Maji wa Nala unaogharimu Sh bilioni 3.8, mradi wa maji wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) unaogharimu Sh bilioni 1.2 na mradi wa maji katika Mji wa Serikali wenye thamani ya Sh bilioni 35.6.

Aidha Aweso alisema Wizara ya Maji kwa kushirikiana na taasisi zake za DUWASA na RUWASA imeunda timu zinazo endelea na mutafiti wa maji chini ya ardhi na uchimbaji wa visima katika maeneo ya Mzakwe, Nzuguni, Kisasa, Nkuhungu,Miganga, Zuzu, Msalato na Ihumwa.

Pia DUWASA inaendelea na taratibu za manunuzi kwa ajili ya mradi wa majisafi kwa maeneo ya Elishadai, Ihumwa na Mahomanyikaambayo inateemewa kuhudumiwa na chazo cha maji cha Nzuguni.

Aidha, Aweso alimuagiza mkandarasi kutekeleza mradi huu ndani ya miezi 7 na si miezi 15 kama ilivyokwenye mkataba kusisitiza kuwa Wizara haitakuwa kikwazo katika utekelezaji wa miradi ya maji katika jiji la Dodoma.

”Mkataba unaonesha mradi utatekelezwa miezi 15, mimi sio mhandisi wa maji lakini nimefanyakazi kwenye sekta hii takribani miaka nane unaenda wa tisa, huu mradi si wa kuutekeleza kwa miezi 15 ni mradi wa kutekelezwa kati ya miezi sita au saba twendeni kwenye uelekeo huo wa kukamilisha mradi mapema watu wanufaike na uwekezaji unaofanywa na mheshimiwa Rais Samia.”

Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde alisema utekelezaji wa mradi wa usambazaji kupitia Nzunguni utasaidia kupunguza adha ya mgao wa maji kwa wananchi wa maeneo ya Nkuhungu, Miganga, Chidachi, Nzuguni, Kisasa-Bwawani,Mwangaza, Ipagala, Ilazo, na Swaswa, Mpamaa na Njedengwa.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde

Awali, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma(DUWASA), Aron Joseph alisema mradi huo utahusisha kuongez ukubwa wa mabomba ya usambazaji maji ambao yataweza kusambaza maji wasatani wa lita milioni 20 kwa siku kwenda maeneo yanayohudumiwa na chanzo hicho.

“Eneo la Nzuguni mpaka sasa lina visima tisa vilivyokamilika ambavyo vinauwezo wa kuzalisha maji lita milioni 20 kwa siku, kwa sasa visima vitano vyenye wastani wa lita milioni 10 ndivyo vimelekezwa kwenye mifumo ya usambazaji, hivyo kwa kutekeleza mradi huu utawezesha visima vinne kuingizwa kwenye mifumo ya usambazaji hivyo kuongeza upatikanaji wa maji.”

Alisema kukamilika kwa mradi huo utaongeza uzalishaji maji kutoka lita milioni 81 hadi 91 kwa siku zawa na ongezeko la asilimia 30 kutoka chanzo cha Nzuguni na kuwahudumi watu wapatao 123,095 na utaleta unafuu wa upatikanaji maji katika maeneo ya Nkuhungu, Miganga, Mkonze, Chidachi na Makulu Ostabeyi.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma(DUWASA), Aron Joseph

“DUWASA inaishukuru Serikali ya awamu ya sita kupitia wizara ya maji kwa kuendelea kipa kipaumbele Dodoma hususani DUWASA katika kutatua changamoto za upatikanaji wa majisafi katika jiji la Dodoma.”

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button