Mongella:Wanawake tumrudishe Samia madarakani

MWANASIASA Mkongwe na mwanaharakati wa haki za Wanawake,Gertrude Mongella amewataka wanawake kumrudisha tena Rais Samia Suluhu Hassan madarakani ili kukamilisha mpango kazi wa kuwainua wanawake.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kusherehekea miaka 30 ya Beijing,Mongela amesema wamrudishe madarakani na wamdai ilani ya mpango kazi na maazimio ya Beijing.

“Ninajivunia sana juzi nilikuwa nje ninaona kufanikiwa na kutoa ukakasi kuhusu Beijing kwasababu rais ni mwanamke,wanawake tusipoangalia hili kama agenda yetu kwamb kuwa na rais mwanamke tumepata bahati.

Ameongeza “Ninaomba Samia arudi ili kuimarisha agenda yetu kuwa mwanamke anaweza na hili nalisema sio kwasababu ya siasa ila uchungu wa Beijing.

Amesema wanawake wasipomchagua Samia wanavunja heshima ya Beijing na pindi atakapomaliza uchaguzi anadeni kwamba wamuulize haiwekani nusu kwa nusu kwa mawaziri na viongozi wengine.

Pia Mongella amesisitiza nchi kuacha kuwa tegemezi huku akiwataka watumie rasilimali na kujitegemea hasa wanawake kutumia elimu zao kuwa wabunifu.

“Utafutwe mkakati wa kuwawezesha watoto wa kike kutengeneza teknolojia na kutumia,elimu ya watu wazima irudushwe jioni twende tukasome TEHAMA na huku ndio dunia inakoenda wajifunze akili mneba,”ameeleza.

Kwa upande Naibu Waziri wa Fedha ,Hamad Chande amewataka wanawake kupendana na kupeana fursa na kusimamia maadili kutokana na mabadiliko ya usasa.

“Matunda ya Beijing ni ongezeko la wanawake katika ngazi za maamuzi na asilimia kubwa ya akinamama wanafanya kazi za kilimo na zingine hivyo wameleta mabadiliko makubwa.

Aidha amewasisitiza wanawake kutoa elimu kwa vijana maeneno ya vijijini wakati huu nchi inapoelekea uchaguzi mkuu wasikubali kuvunja amani ya nchi.

Naye Prof Penina Mlama kutoka Women Fund Tanzania-Trust amesema mkutano wa Beijing umebadilisha Dunia kwasababu serikali zote hazikuwa na hiari bali waliingiza kwenye sera na kuketa usawa wa kijinsia.

“Tukumbuke mkutano huu ulikuwa muhimu kwetu tumpe hongera mama Mongella kwa kuendesha mkutano kwa umakini kwani walitoka na tamko moja linalozimgatia matakwa ya ulimwengu wote.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button