Amnesty yabaini ukandamizaji wa haki za binadamu Msumbiji

MSUMBIJI : SHIRIKA la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu, Amnesty International,limetangaza kwamba vikosi vya usalama vya Msumbiji viliendesha operesheni za ukandamizaji kwa karibu miezi mitatu baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Katika taarifa yake, Amnesty imewanukuu watetezi wa haki za binadamu wakisema kwamba ukandamizaji huo ulisababisha vifo vya zaidi ya watu 300. SOMA: Amnesty yaitaka Mali kuchunguza mauaji ya raia

Amnesty imezitaka mamlaka za Msumbiji kuchunguza mauaji haya na ukiukaji wa haki za binadamu ulioshuhudiwa, na pia kutoa wito kwa wale waliohusika kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Maelfu ya watu walikuwa mitaani wakipinga matokeo ya uchaguzi ambapo Daniel Chapo wa Chama tawala cha Frelimo alitangazwa mshindi, huku mgombea wa upinzani, Venancio Mondlane, akidai uchaguzi huo ulikumbwa na dosari na madai ya wizi wa kura.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button