Wananchi kijiji cha Msilili Newala kunufaika na zahanati ya bil 1/-

MTWARA: WAKAZI wa kijiji cha Msilili kata ya Mcholi II Halmashauri ya Mji Newala mkoani Mtwara wanategemea kunufaika na mradi wa zahanati uliogharimu zaidi ya Sh bilioni 1.

Akizungumza katika halmashauri hiyo  wakati Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025 ulipozindua mradi huo, Diwani wa Kata ya Mcholi II, Majidi Amri amesema kwa sasa wananchi wataondokana na changamoto ya huduma hiyo iliyokuwa ikiwakabili kwa muda mrefu.

“Mpaka sasa tunauzindua huu mradi wananchi wamefurahi kufanikisha mradi huu kwa kushirikiana na sisi viongozi kwasababu utawapunguzia adha ya kwenda vijiji irani kufata huduma hii,” amesema Majidi.

Amesema mradi huo utanufaisha wananchi wa kijiji hicho cha msilili ambako mradi upo pamoja na vijiji vingine vinavyozunguka eneo hilo la mradi ambapo umefadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Nchini (TASAF).

SOMA ZAIDI: Mwenge wa Uhuru watua Mtwara

Mkazi wa kijiji hicho, Sofia Maico ameipongeza serikali kwa kuwaletea huduma hiyo karibu kwani imewapunguzia akina mama hao usumbufu waliyokuwa wakiupata awali hasa wakati wa kujifungua ambapo walikuwa wakiipata vijiji jirani ikiwemo mkunya.

Mbunge wa Jimbo la Newala Mjini ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum) Kapteni Mstaafu George Mkuchika amewapongeza wakazi hao kwa jitihada kubwa waliyoonyesha katika mchakato mzima wa ujenzi wa zahanati hiyo.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ali Ussi amewataka wananchi kutunza miundombinu ya miradi yote inayotekelezwa kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Mbali ya miradi huo wa zahanati, miradi mingine iliyopitiwa na mwenge wa uhuru kwenye halmashauri hiyo ikiwemo ujenzi wa uendelezaji mradi wa ujenzi wa barabara ya makondeko – kiuta –mkunya yenye urefu wa kilomita 1.5 kiwango cha lami.

Ujenzi wa nyumba ya watumishi katika shule ya sekondari tulindane, ukarabati wa mradi wa maji chiunjila na mingine huku ukikimbizwa umbali wa kilomita sabini na tano kwenye tarafa mbili, kata kumi, mitaa mitano na vijiji kumi na tatu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button