Wadau 800 nchi 40 duniani kushiriki maonyesho KKF

ARUSHA: ZAIDI YA wadau 800 wa utalii kutoka nchi 40 duniani wanatarajia kushiriki maonesho ya kimataifa ya Karibu- Kilifair Ltd (KKF) yanayotarajiwa kufanyika Juni 6 hadi 8 mwaka huu mkoani Arusha.
Lengo ni kuvutia watalii wengi zaidi na kuinua uchumi wa nchi.

Akizungumza jijini Arusha, Mkurugenzi wa Kilifair Ltd, Dominic Shoo amesema maonesho ya Karibu -Kilifair (KKF) yamekuwa yakifanyika kila mwaka na yanalenga kutangaza na kukuza utalii nchini na kwa mwaka huu yatakutanisha makampuni mbalimbali ya utalii zaidi ya 500 ya ndani na nje ya nchi.

” Tumelenga kutangaza utalii ndani na nje ya nchi hasa nchi za Afrika Mashariki EAC na tumeleta mwaka huu wadau wa utali wasiopungua 800 kutola sehemu mbalimbali duaniani na zaidi ya nchi 40 zitashiriki pamoja na zaidi ya makampuni 500 yatapata fursa ya kutangaza bidhaa zao za utalii,”.
Shoo amesema maonesho hayo yamekuwa na manufaa makubwa kwa washiriki kujifunza na kujionea vivutio mbalimbali nchini na kuwa mabalozi wazuri wa kuleta watalii nchini kutoka mataifa mbalimbali duniani.



