Hazina, wawekezaji kudumisha ushirikiano

DAR ES SALAAM :MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu amesema serikali itaendelea kushirikiana na wawekezaji na kudumisha ushirikiano ili kuwa na tija na manufaa kwa taifa.
Mchechu amesema hayo Mei 27, 2025 jijini Dar es Salaam alipotembelea na kampuni ya Puma ambapo walijadili ushirikiano na uwekezaji na kuongeza kuwa Puma inamilikiwa na serikali kwa asilimia 50 na wawekezaji asilimia 50.
SOMA ZAIDI: Mchechu achangisha mil 117.8/- ujenzi wa kanisa – …
Aidha, Nehemiah amesema Tanzania itaendelea kufanya mageuzi na kuboresha rasilimali zake ili nchi iweze kunufaika nazo ikiwa ni pamoja na mazai ya kampuni ya Puma kama nishati ili kuzalisha faida na mapato mara mbili zaidi .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Puma Duniani, Marc Russel amesema anajivunia kuwa Afrika hususani Tanzani kwani ni sehemu muhimu ya kuwekeza kubiashara na kuna fursa mbalimbali .
Naye, Mkurugenzi wa Puma, Fatma Abdallah amesema tanzania inaongoza kwa mapato, faida na ni nchi ya kimakakati kwao ili kuona kuendeleza mashirikiano ya pande zote mbili.



