Makandarasi wazawa hupewa tuzo wakifanya vizuri

DODOMA; SERIKALI imesema makandarasi wazawa wanaofanya vizuri hupatiwa tuzo mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Bukoba Mjini,Stephen Byabato aliyetaka kujua serikali imeweka utaratibu gani kuwatambua makandarasi wazawa wanaofanya kazi nzuri ili kuwapa motisha.

“Serikali kupitia Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) huwatambua Makandarasi wanaofanya kazi nzuri kwa kuwapatia tuzo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na tuzo za ukuaji haraka kwa wale wanaoonyesha ukuaji mzuri tangu usajili.

“Tuzo kwa wakandarasi wanaozingatia usalama kazini na tuzo kwa ajili ya kumpuni zinazomilikiwa na wanawake zenye mafanikio katika miradi.

“Aidha, Mkandarasi anapokamilisha kazi aliyopewa vizuri kulingana na mkataba mwajiri hutoa hati maalum ya kukamilisha kazi (Final Completion Certificate), ambayo hutambua kuwa kakamilisha kazi yake vizuri,” amesema Naibu Waziri.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button