Muda wa kusoma bajeti kuu kuwekwa kwenye kanuni

BUNGE leo Juni 11, 2025 limepitisha mapendekezo ya maboresho ya Kanuni za Kudumu za Bunge, ambapo miongoni mwa maboresho hayo ni kutambua muda wa kusoma Bajeti ya serikali kwamba ni saa 10:00 jioni.
–
Mapema leo asubuhi, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni za Bunge, Mussa Azzan. aliwasilisha taarifa ya kamati hiyo kuhusu Marekebisho au mabadiliko katika Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Februari 2023.
–
“Uzoefu umeonyesha kuwa Bajeti Kuu ya Serikali imekuwa ikisomwa saa 10:00, jioni lakini muda wa kusoma bajeti haupo katika kanuni ya 124 inayosimamia suala hilo.
–
“Kamati inapendekeza yafanyike marekebisho ili kutambua muda wa kusoma bajeti ya serikali kwamba itakuwa ni Saa 10:00 jioni, lakini vilevilie kuwezesha kuendana na makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kusoma bajeti zao kuu za serikali kwa pamoja wakati huo,” amesema.