Mfumuko wa bei wapungua

DODOMA; Mfumuko wa bei nchini ulipungua na kufikia asilimia 3.1 mwaka 2024 ikilinganishwa na asilimia 3.8 mwaka 2023, Bunge limeelezwa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema hayo bungeni leo, alipokuwa alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi kwa Mwaka 2024 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2025/26.

“ Mfumuko wa bei ulipungua kutokana na usimamizi madhubuti wa sera za fedha na bajeti, kutengemaa kwa bei za mafuta katika soko la dunia na kuimarika kwa upatikanaji wa chakula katika masoko ya ndani.

“ Kiwango hiki cha mfumuko wa bei kipo ndani ya wigo wa lengo la Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ya kutokuzidi asilimia 8.0 na kuwa kati ya asilimia 3.0 hadi 7.0, mtawalia,” amesema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button