Misingi ya bajeti 2025/26 hii hapa

DODOMA; WAZIRI wa Fedha, Dk Mwiguku Nchemba, muda huu anawasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2025/26.

“Kwa kuzingatia mwenendo wa viashiria mbalimbali vya uchumi jumla na utekelezaji wa bajeti ya Serikali, shabaha na malengo ya uchumi jumla kwa mwaka 2025/26 ni kama ifuatavyo:

“ Kuongeza kasi ya ukuaji wa Pato Halisi la Taifa kufikia asilimia 6.0 mwaka 2025 kutoka ukuaji wa asilimia 5.5 mwaka 2024;

“ Kuendelea kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kuhakikisha kuwa unabaki kwenye wigo wa tarakimu moja ya wastani wa asilimia kati ya 3.0 – 5.0 katika muda wa kati;

“ Mapato ya ndani kufikia asilimia 16.7 ya Pato la Taifa mwaka 2025/26 ikilinganishwa na asilimia 15.8 mwaka 2024/25;

“Mapato ya kodi kufikia asilimia 13.3 ya Pato la Taifa mwaka 2025/26 kutoka asilimia 12.8 mwaka 2024/25; 69.

“ Nakisi ya bajeti (ikijumuisha misaada) kuwa asilimia 3.0 ya Pato la Taifa mwaka 2025/26 kutoka asilimia 3.4 mwaka 2024/25; na

“ Kuwa na akiba ya fedha za kigeni kwa kiwango cha kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kisichopungua miezi minne,” amesema Waziri Nchemba.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button