Tanzania, Marekani zashauriana changamoto za uhamiaji

SERIKALI ya Tanzania imeanza mashauriano na Serikali ya Marekani kuhusu masuala ya uhamiaji ambayo yanaweza kuathiri raia wa Tanzania kuingia nchini humo.

Uamuzi huo unatokana na Marekani kupanga kuongeza orodha ya mataifa yaliyopigwa marufuku raia wake kuingia nchini humo, ikiwemo Tanzania.

Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa katika taarifa yake alisema Tanzania imepata taarifa hiyo na tayari imeanza mazungumzo na Serikali ya Marekani kupitia Wizara ya Mambo ya Nje kufahamu kikamilifu maeneo ambayo yanapaswa kurekebishwa.

“Serikali imeona Tangazo la Serikali ya Marekani la kutaka kufanyiwa kazi kwa mambo kadhaa ya kiuhamiaji ambayo yanaweza kusababisha raia wa Tanzania kuzuiwa kuingia Marekani,” alisema Msigwa kupitia taarifa yake na kuongeza:

“Tayari Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje imeanza kufanya mashauriano na wenzetu wa upande wa Marekani kujua maeneo ambayo yanatakiwa kufanyiwa maboresho hususani yanayohusiana na masuala ya kikonseli ili kuharakisha Tanzania isiwe moja ya nchi ambazo raia wake watazuiwa kuingia Marekani”.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button