Uchache vituo vya nishati, chanzo kuuza mafuta kwenye madumu

SONGWE: UCHACHE wa vituo vya mafuta na usambazaji wa gesi ya kupikia hususa ni katika maeneo ya vijijini katika mkoani wa Songwe kunatajwa kuwa ni miongoni mwa changamoto kubwa inayopelekea wananchi kukiuka sheria na taratibu kwa kuuza mafuta kwenye chupa  na madumu vinavyotajwa kuwa na athari kiafya, kiuchumi na kimazingira.

Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Farida Mgomi katika ufunguzi wa kikao cha wadau wa mafuta na gesi ya kupikia juzi katika kata ya Itumba wilayani Ileje.

Amesema pamoja na  jitihada kubwa zinazofanywa na Rais wa Samia Suluhu Hassan kulisimamia suala la mkakakati wa taifa wa matumizi ya nishati ya kupikia (2024-2034). kuhakikisha matumizi ya nishati safi kuweza kuwafikia watanzania asilimia 80% ifikapo mwaka 2034.

Amesema kwa upande wa mkoa wa Songwe bado kuna uhaba mkubwa kwani vipo vituo vya mafuta 59 pekee ambapo vinne kati ya hivyo vikiwa maeneo ya Vijijini.

“Kwa upande wa Wilaya za Mkoa wa Songwe mgawanyiko wa vituo vya mafuta ni kama ifuatavyo upande wa Wilaya ya Ileje Kuna vituo vituo viwili ambavyo vipo mjini , Wilaya ya Mbozi vituo 23 kati ya hivyo viwili vipo kijijini, Momba vituo 29 kati ya hivyo ni viwili pekee ambavyo vipo vijijini na upande wa wilaya ya Songwe Kuna vituo vitano ambavyo vyote vipo mjini,” amesema Mgomi.

Mgomi amewataka EWURA kuongeza kasi ya elimu na kutoa leseni kwa waagizaji na wasambazaji wa gesi inayotokana na mafuta ya petrol ,.. ameongeza kuwa  kwa upande wa gesi ya kupikia katika mkoa wa Songwe Kuna msambazaji mmoja tu wa gesi ya kupikia licha ya uhitaji kuwa mkubwa.

“Kuwepo kwa msambazaji mmoja wa gesi ya kupikia, hii ni tafsiri kuwa huduma za gesi ya kupikia (LPG) Bado hazitoshelezi hapa Ileje na mkoa wa Songwe kwa ujumla , hivyo ni dhahiri kuwa hili linahitaji msukumo ili kusogeza na kuimarisha utoaji wa huduma inayoakisi upatikanaji nishati safi ya kupikia kwa kila mtanzania,” alieleza Mkuu wa Wilaya.

Meneja wa Ewura Kanda ya Mbeya inayojumuisha mikoa ya Songwe, Mbeya , Njombe, Ruvuma na Rukwa Karim Ally amesema kutokana na wilaya ya Ileje miundombinu yake kuanza kufunguka hasa barabara wakishirikiana na uongozi wa wilaya wameanza kujikita kutoa elimu kwa wafanya biashara ikiwa ni pamoja kuwafundisha namna ya kuomba utaratibu wa kuomba vibali na leseni kwa vituo vya mafuta mjini na vijijini pamoja na vibali vya usambazaji gesi ya kupikia.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button