Mwenyekiti INEC aeleza waratibu waliyojifunza kuelekea uchaguzi

SHINYANGA: MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ( INEC )Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele amesema sheria mbili mpya waliyojifunza waratibu ,wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo ni kupiga kura moja ya Rais nje ya vituo kwa waliojiandikisha na namna ya kusimamia uchaguzi kwenye maeneo yenye mgombea mmoja na kusimamia maeneo ya Magereza kwa kuyazingatia.
Ambapo Sheria ya Uchaguzi wa Rais ,wabunge na madiwani namba moja ya mwaka 2024 na Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Namba 2 ya 2024.
Jaji Mwambegele amesema hayo leo alipofungua mafunzo hayo kwa watu hao ngazi ya jimbo pamoja na maafisa manunuzi huku akieleza jukumu lililobaki kwao ni kutoa mafunzo sahihi kwa kuonyesha kwa vitendo.

Jaji Mwambegele amesema kupiga kura ya Rais nje ya kituo kwa waliojiandikisha na namna ya kusimamia uchaguzi kwenye maeneo yenye mgombea mmoja na Magerezani ni moja ya mambo machache ambayo hayakuwepo kwenye sheria zilizopita na hakuna mwenye uzoefu nayo.
“Leo mmehitimu mkiwa na kazi kubwa mbili mnazopaswa kuzitekeleza namba moja ni kutoa mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wa uchaguzi ngazi ya kata na mtayaratibu vizuri kwa weledi na mbili mtayatafsiri mafunzo kwenye usimamizi wenu,” amesema Jaji Mwambegele.
Jaji Mwambegele amesema wahakikishe pia shughuli za masuala ya uchaguzi kuanzia vikao na vyama vya siasa ,utoaji fomu za uteuzi na wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani unafanyika kwa mujibu wa sheria.

Jaji Mwambegele amesema katika maeneo mbalimbali yaliyopita wakati wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kulitokea changamoto ya kutobandikwa mabango yaliyopaswa kubandikwa yanayoelezea sifa ya mtu kuwa mpiga kura.
“Niwakumbushe kuwa ubandikaji wa Mabango,orodha ya majina ya wapiga kura na matangazo au taarifa ni takwa la kisheria na kanuni zinazo simamia uchaguzi”amesema Jaji Mwambegele.
Pia Jaji Mwambegele amesema hivi sasa yapo makundi sogozi au ya WhatsApp ambayo aliwatahadharisha kwa kipindi hiki wayapunguze kuyatumia ili wasije kukosea kutuma taarifa ya aina yoyote katika makundi hayo ambayo hayapaswi kutumwa huko.
Jaji Mwambegele amesema kuhusu taasisi binafsi zinazotoa elimu kuhusu masuala ya uchaguzi wajirizishe kwanza kama wamepewa kibali na Tume na wamepangiwa kutekeleza majukumu hayo.



