Takwimu zatakiwa wenye magonjwa yasiyoambukiza

DAR ES SALAAM :WAHUDUMU wa afya ngazi ya jamii wamehimizwa kuandaa takwimu za wagonjwa wanaoishi na magonjwa yasiyoyakuambukiza lengo likiwa ni kuweka uelewa dhidi ya magonjwa hayo na kuyapa kipaumbele.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam Dk Anna Nswila kutoka Chama cha Wagonjwa wa Kisukari kwenye mafunzo maalumu ya uelewa dhidi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza (NCDs) iliyoandaliwa na Shirikisho la Vyama yasiyo ya Kuambukiza Tanzania (TANCDA.
“Wahudumu ngazi ya jamii ni muhimu sana kwani wao ndio watu wa kwanza kuwa karibu na wananchi katika jamii wanayoishi kuliko mtaalamu mwingine wa sekta ya afya ukiangalia jinsi walivyo na majukumu yao waliyopewa kwanza katika kila kata kuna wawili, kuna mwanaume mmoja na mwanamke mmoja.”
“Lakini wote pia wamepewa elimu ya kuwahudumia wananchi au kuwashauri kuhakikisha kuwa katika matatizo yao wanapelekwa katika vituo vya kutolea huduma kwa ukaribu wa zahanati, kituo cha afya mpaka kufika kwenye ngazi ya rufaa maana rufaa ya kwanza ni zahanati kutoka kwao,”
“Muhudumu ngazi ya jamii anapaswa ajue ana idadi ya wagonjwa hawa katika hao kuna wagonjwa wenye magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni idadi hii anatakiwa ajue na wagonjwa wenye kisukari wangapi, wenye saratani wangapi baada ya kujua hiyo idadi anaweza sasa kufahamu na kutoa mrejesho kwao na kuwashauri kwanza sio wewe peke yako mpo watano sita na huyu mwenzako alikuwa na dalili za aina hii lakini mpaka sasa hivi ameweza kupata matibabu,”amesema Dk Anna.
Kwa upande wake Zuhura Ngogoto mhudumu ngazi ya afya kutokea Chamazi amesema wanakutana na changamoto bado nikubwa kwa jamii juu ya watu wanaoishi na magonjwa yasiyoya kuambukiza hivyo elimu inapaswa kutolewa zaidi jamii iweze kupa uelewa.
Kwa upande wao baadhi ya watu wanoishi na magonjwa yasiyo ya kuambukiza Aziz Mbwana Na Saraphina Adam wamesema jamii imekuwa na uekewa mdogo kwani imekuwa ikichukulia magonjwa hayo ni kama ushirikina hivyo inapaswa kuelimishwa zaidi.



