“Kumpa mtoto Iphone sio malezi”

BUKOBA: WAZAZI na walezi katika Halmashauri ya Bukoba wametakiwa kuhakikisha wanatanguliza eliku kwa watoto wao kuliko kufikiria kutoa vitu vya gharama kama simu aina ya Iphone ili kuwafurahisha.

Wito huo umetolewa leo Julai 23, 2015 na Ofisa Elimu ya Msingi wa Halmashauri ya Bukoba, Julius Shulla wakati akizungumza na wazazi kwenye mahafari ya 14 ya Shule ya Msingi ya Rweikiza.

Amesema kuwa kuwa imekuwa kasumba kwa wazazi kuweka mawazo yao juu ya kufurahisha watoto wao kuliko kufikiria namna ya kuwapa elimu bora.

“Nimeona wazazi wakitafuta pesa ya Iphone,pesa ya zawadi nono kwa ajili ya zawadi za watoto wao kuliko kufikiria juu ya Kutafuta elimu kwa watoto wao ,wito wangu wekeza juu ya watoto kwa sababu elimu ndio kitu pekee kinachoweza kuwasaidia watoto wenu nyingine ni mbwembwe,”amesema Shulla.


Baaadhi ya wazazi walivutiwa na ujumbe huo akiwemo Clementina Ruyango kuwa amekuwa akisomesha watoto wake kwa matamanio kuwa siku moja wajiajili na wawe sehemu ya msaada kwa jamii.

Mkurugenzi wa shule, Jasson Rweikiza amesema kuwa shule hiyo imekuwa kivutio kwa wazazi wengi wa Bukoba vijiji kutokana na Kuwa na ufahulu mzuri huku akidai kuwa shule hiyo imeweka mazingira mazuri ikiwemo vifaaa vya kisasa vya kidigatal vya kijufunzia vinavyokuza uelewa kwa watoto wadogo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button