Mtoto wa Kombani kinara ubunge viti maalum

MOROGORO: WAJUMBE wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Uchaguzi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro wamempa kura 1,314 Lucy Simirya Kombani na kuongoza kwenye kinyang’anyiro cha ubunge wa Viti Maalum mkoa wa Morogoro dhidi ya wagombea wenzake wanane .
Msimamizi mkuu wa uchaguzi huo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima alitangaza usiku wa Julai 30, 2025 baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu kura katika uwanja wa Jamhuri wa Morogoro.
Malima amesema katika mkutano mkuu maalumu wa uchaguzi huo ulihudhuriwa na wajumbe 1,653 , kura saba (7) ziliharibka na kura halali zilikuwa 1,646.

Malim amemtaja Lucy Simirya Kombani ameongoza dhidi ya wenzake nane kwa kupata kura 1,314 , nafasi ya pili imechukuliwa na Sheila Lukuba aliyepata kura 597 , Lukuba aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro.
Amewataja wengine na kura zao kwenye mabano ni Josephine Kupuna (454), Jane Claude Mihaji ambaye kitalauma ni Mwandishi wa habari Mwandamizi (339) Aliyah Awadh Omar (236), Amina Ally Karuma (153), Mwalimu Hajira Said Mwikoko (90), Dk Kulwa Nuhu Kangeta (75) na Rahel Stephen Mashishanga (35).

Akizungumza baada ya matokeo hayo Lucy ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Tamisemi , Celina Kombani ameeleza ya kwamba zoezi upigaji kura lilienda vizuri na wote wameridhika na matokeo .
Amesema yeye ni kijana ambapo Rais Dk Samia Suluhu Hassan amekuwa wakiwaamini vijana na unapoaminiwa ni vyema uaminike ,hivyo amejipanga na yupo tayari kusiammia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.



