“Wenye kifafa wasitengwe”

DAR ES SALAAM: WATANZANIA wameshauriwa kuacha tabia ya kuwatenga watu wenye kifafa kwani wanapaswa kupata haki sawa kama wengine.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam na Suzana Mukoyi wakati akimwakilisha Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Epilepsy Organisation walipokutana wanachama hao wakizindua mradi wao wa Ongea Simama Imara wenye lengo la kuhakikisha watu wanaolea watoto wenye kifafa wanajua haki yao ya msingi na kutatua changamoto hizo.

Aidha, Suzana amesema mradi huo wanampango wa kufikia nchi nzima huku wakiwa wameanza na mkoa wa dar es salaam ambapo amesema kwenye taasisi hiyo wamefikisha wanachama 1,000 na uelewa wa ugonjwa huo wa kifafa ni mkubwa kwa sasa ukilinganisha na hapo awali.

Naye Rebecca Hudson Lebi Mwanachama wa Taasisi ya Tanzania Epipsy Orgenisation ametoa wito kwa jamii na serikali kuhakikisha wanapata bima ya afya ili kuweza kuwarahisishia kupata matibabu kwa urahisi kwani kuna baadhi ya dawa ni ngumu kuzipata kwenye bima.

Nao wahanga wa ugonjwa huo wa kifafa Omary Vadenga na Elias Manade wamesema taasisi hiyo ina mchango mkubwa kwao kwani imewajengea uwezo mkubwa kwa kujua changamoto zao kadri siku zinavyozidi kwenda hivyo na kutoa wito kwa jamii isiwatengee iwape kipaumbele kama watu wengine

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button