FCT watakiwa kutafakari mashauri ya rufaa

BARAZA la Ushindani (FCT) limeagizwa kutafakari kwa kina maamuzi ya mashauri ya rufaa yanayogusa maisha ya watu kwa maslahi ya ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla ambayo yanaweza kubadili mwelekeo wa kiuchumi.

Agizo hilo limetolewa leo jijini Arusha na Mkurugenzi wa Sera , Mipango na Utaribu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Needpeace Wambuya kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk,Hashil Abdalah katika ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wajumbe wapya wa bodi hiyo.

Amesema azma ya serikali ni kuhakikisha uchumi wa nchi unaimarika zaidi kupitia uwekezaji kwenye viwanda uendeshaji wa biashara kwa njia ya haki ikiwemo umuhimu wa kumpa nafuu mlaji.

“Baraza hili lilianzishwa kwa lengo la kumlinda mlaji katika soko ikiwemo ukizaji wa uchumi hivyo haki itakayotolewa na baraza hili kutakuza ubunifu na tija katika soko ikiwemo ukuzaji wa mitaji toeni maamuzi kwamujibu wa sheria na ushahidi uliowasilishwa”

Amesisitiza taifa linapaswa kuwa na uchumi wa sh, trilioni 1 hivyo lazima kuwa na mazingira yatakayochagiza maendeleo kwa kuhakikisha wanazingatia vipaumbele vilivyoanishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025-2030 ikiwemo kuhakikisha kuendelea kujenga uchumi imara kupitia uwekezaji na viwanda sanjari na ulinzi usalama.

Naye, Mwenyekiti wa baraza hilo, Jaji Rose Ebrahim amesisitiza kuwa mafunzo hayo wanayopewa yanalengo la kuwaongezea uwezo katika ufanisi wa kazi na kutoa maamuzi sahiho pindi watakapopitia majalada yaloyowasilishwa kwaaajili ya maamuzi katika kuleta tija ya biashara nchini

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button