Wakulima wapewa amri 8 za kilimo cha kahawa

BUKOBA: Taasisi ya Utafiti ya Kahawa mkoani Kagera (TACRI) imewapa elimu wakulima wa kahawa mkoani humo huku ikiwapa amri nane za kuongeza tija la zao hilo.

Aidha, lengo ni kuzalisha tani 200,000 ifikapo mwaka 2030.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Kanda ya Kagera, Dk Nyabisi Ngho,ma amesema utafiti uliofanywa kwa wakulima wa zao la kahawa mwaka 2006 kupitia taasisi hiyo ulibaini kuwa kama wakulima watafuata kanuni na amri hizo mche mmoja unaweza kuzalisha kahawa safi kilogramu 2.5 hadi 3.5.

Amesema baada ya utafiti huo serikali na wadau wa kahawa walianza kuchukua hatua hadi kufikia jitihada za kuongeza uzalishaji mwaka 2021 ambapo baadhi ya wakulima wapo wanaozalisha kilogramu 4 kwa mche mmoja ingawa ni wachache.

Kupitia maonesho ya Nanenane mwaka huu yameweka darasa na mafunzo madhubuti za kumfundisha Kila mkulima atakayeingia katika Banda hilo atasoma bango na kupata darasa la amri nane za kuongeza tija katika kilimo cha kahawa.

“Bango ni kubwa mwitikio wa wakulima ni mkubwa sana, hii ni madhubuti kwa wakulima wote wa Kahawa kuhakikisha wanavuka hapo walipo mfano mwanzoni ilikuwa mkulima wa kahawa anavuna gramu 3 kwenye mti mmoja lakini kwa sasa baadhi wanaozingatia wanavuna kilogramu 4 kwa mche na wasiozingatia wanasababisha mkoa wa Kagera kupoteza mabilioni ya pesa,” amesema Ngh,oma.

Amesema zao hilo linaweza kubadili uchumi wa mtu mmoja mmoja ambapo alidai kuwa mpaka sasa wakulima wanamiche milioni 51,000 na kama wangezingatia kilimo bora mkoa ungekuwa unavuna tani 127,000 za kahawa safi na kuingiza mabilioni ya fedha nyingi ambazo zingemjenga mwananchi mmoja mmoja na Kusaidia viwanda vinavyoongeza thamani kuchakata bidhaa za zao hilo mwaka mzima.

Amesema pia changamoto nyingine ni mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo baadhi ya sehemu mvua zinachelewa kunyesha hivyo kahawa inayoota maarufu kama ndagashe inakiwa haina ubora unaotarajiwa na kupelekea zao hilo bei kushuka .

Aliizitaja amri hizo kuwa ni kukata matawi vizuri, kudhibiti magonjwa na wadudu, kuweka mkazo kwenye lishe ya miti ya kahawa, kufanya palizi shambani, kuhakikisha wanaondoa maotea mara kwa mara, kuweka matandazo vizuri ili kupata faida ya unyevunyevu,kumwagilia maji inapowezekana kama jua ni kali sana pamoja na kupangilia kivuli kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button