Vijiji zaidi ya 30 kupitiwa mradi uchukuaji taarifa za mitetemo

MTWARA: ZAIDI ya vijiji 30 katika Mkoa wa Mtwara vitapitiwa na mradi wa uchukuaji taarifa za mitetemo kwenye kitalu cha utafutaji wa mafuta na gesi asilia Lindi – Mtwara unaotekelezwa na Shirikia la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Hayo yamejiri wakati wa ghafla fupi ya kuutambulisha mradi huo wa uchukuaji taarifa za mitetemo kwenye kitalu cha utafutaji wa mafuta na gesi asilia Lindi – Mtwara, iliyofanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.

  • Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala amesema shughuli hizo pamoja na kwamba zina faida kwa serikali kwa ujumla lakini lazima ziwanufaishe wanamtwara kwa kupata ajira za muda mfupi pamoja na fursa ya kufanya biashara kutokana na uwepo wa wageni mbalimbali katika maeneo yao ikiwemo ya vyakula, hoteli na zingine.

‘’Kikubwa zaidi niwaombe wananchi kutoa ushirkiano kwa wenzetu wa TPDC ili dhamira njema ya serikali yetu kuhakikisha rasilimali zilizopo katika nchi yetu zinatusaidia, itakuwa ni muhimu ushirikiano kwa ngazi zote viongozi, wananchi na kila mmoja wetu ili nia njema hii iweze kutimia’’amesisitiza Sawala

Mtaalam wa Miamba Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia wa Uchukuaji Taarifa za Mitetemo Kitalu cha Lindi – Mtwara, Venance Emmanuel amesema mradi huo unalenga kutafuta rasilimali ya mafuta na gesi asilia chini ya ardhi kisha kuwawezesha kutafsiri taarifa hizo na kugundua mahali ambapo kuna uwezekano wa uwepo wa rasilimali hiyo.

Pia mradi kwa sehemu kubwa kwa mkoa wa mtwara unachukuwa takribani vijiji hivyo 30 na eneo la Lindi unagusa vijiji zaidi ya 8 katika wilaya ya Mtama huku akiwataka wananchi wa maeneo hayo kukwepa suala la udanganyifu hasa wakati wa tathimini na fidia.

Aidha baada ya ugunduzi ya rasilimali hiyo kutakuwa na faida za muda mrefu ikiwemo nchi kunufaika na mambo mbalimbali kama vile upatikanaji wa nishati nchini hasa ikizingatiwa kipindi hiki asilimia kubwa nchi inatumia nishati itokanayo na gesi asilimia kwa takribani asilimia 60.

‘’Ufatutaji huu unajaribu kuongeza wingi wa nishati ya gesi ili tuweze kuwa na uhakika zaidi ya upatikanaji wa nishati, faida nyingine endapo tutaweza kugundua pia utaboresha huduma mbalimbali za wananchi ikiwemo hospitali, barabara, elimu na mapato yatakayotokana na nishati hii yataongeza upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutoa huduma katika maeneo  hayo’’amesema Venance

Mradi huo unaambatana na fursa mbalimbali za muda mfupi na za muda mrefu na faida za muda mrefu ni katika mazingira ambayo kazi hiyo inafanyika kazi ikiwemo ajira za wenyeji wataokuwa wanasaidia kutengeneza barabara zitazokuwa zinatumiwa na mitambo hiyo ya uchukuaji wa taarifa za mitetemo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button