Buriani Ndugai

DAR ES SALAAM; SPIKA mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai(62) amefariki dunia jana jijini Dodoma.
Ndugai ambaye pia alikuwa Mbunge wa Kongwa alizaliwa Januari 22, 1963 katika Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma na safari yake ya kisiasa ilianzia mwaka 2000 alipogombea na kushinda ubunge wa Jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika safari yake ya kisiasa Ndugai aliendelea kukua baada ya 2005 hadi 2010 kuwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na baadaye kuiongoza kamati hiyo hadi mwaka 2010 alipochaguliwa kuwa Naibu Spika wa bunge chini ya Spika wa wakati huo Anne Makinda.
Katika Uchaguzi Mkuu 2015, Novemba 15, 2015 Ndugai alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge la 11 na mwaka 2020, alirejea tena bungeni na kushika nafasi kama spika kwa kura nyingi, hata hivyo Januari 6, 2022, alitangaza kujiuzulu katika nafasi yake ya uspika na alisalia kuwa Mbunge wa Jimbo la Kongwa.
Hadi umauti unamkuta Ndugai alikuwa ameshinda kura za maoni katika mchakato wa kumpata mgombea wa ubunge wa Jimbo la Kongwa na kuibuka mshindi kwa kura kura 5,690 akiwashinda Ngaya Mazanda 195, Emmanuel Mbena 232, Pascal Mahinyila 321, Philipo Chiwanga 358, Elias John 435, Simon Ngatunga 517, Samora Mshana 544, Deus Seif 1,260 na Isaya Mbulumi 2,602.
Aidha kufuatia kifo cha Ndugai, Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pole kutokana na kifo hicho.
Kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa X, Rais Samia alitoa pole kwa familia, wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), watumishi wa Bunge na wabunge wote aliotumikia naye akiwa Spika wa Bunge, wananchi wa Kongwa, ndugu, jamaa na marafiki.
“Tuungane pamoja kumuombea kwa Mwenyezi Mungu na kuiombea familia, ndugu, jamaa na marafiki uvumilivu, faraja na moyo wa ibada katika kipindi hiki kigumu. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi,” alieleza Rais Samia.
Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ametoa salamu za pole kwa Rais Samia, Dk Tulia, familia ya marehemu, wananchi wa Jimbo la Kongwa, ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huo.
Taarifa ya Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Raqey Mohamed ilieleza kuwa Dk Mwinyi anamkumbuka Ndugai kwa mchango wake katika nyadhifa mbalimbali za uongozi.
Awali, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alitangaza kifo cha Ndugai.

Taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma katika Ofisi ya Bunge, ilieleza mwanasiasa huyo mkongwe aliaga dunia jijini Dodoma jana.
“Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa Jimbo la Kongwa, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” alisema Dk Tulia.
Taarifa ilieleza Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na kamati ya mazishi na familia ya marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.
Katika hatua nyingine, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa pole kwa Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, familia na wananchi wa Kongwa kutoka na kifo cha Ndugai.
Taarifa ya Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk Emmanuel Nchimbi ilieleza CCM imepokea kwa mshtuko na masikitiko taarifa za kifo cha kiongozi huyo.
“Tumempoteza mwana CCM mwenzetu, kiongozi shupavu, mzalendo wa kweli na mtumishi mahiri wa umma ambaye alitoa mchango mkubwa katika kuimarisha taasisi ya bunge,” alisema Dk Nchimbi.
Alisema CCM itamkumbuka kwa uadilifu wake, uthubutu na moyo wa kizalendo alioutoa wakati wote wa utumishi wake kwa chama na taifa kwa kusimama imara katika kulinda maslahi ya umma na kuendeleza utawala wa sheria.
Wakati wa kumalizika kwa Mkutano wa 19 wa Bunge la 11 Ndugai aliitambulisha familia yake akiwemo mkewe Dk Fatma Mganga na watoto wao watatu.
Kiongozi huyo alimshukuru mkewe kwa kumhudumia hata alipolazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) nchini India.
“Kuna wakati alikuwa analala hapo pembeni ya kitanda changu saa 24 amekaa kwenye kiti, nilikuwa naumwa sana kiasi ambacho kwa kawaida mtu haruhusiwi mtu ambaye sio mhudumu wa hospitali ile kukaa kwa maana ya wodi ile maalumu lakini ikabidi yeye aruhusiwe kukaa mle ndani na mimi, akilala kwenye kiti saa 24 kwa siku kadhaa,” alisema Ndugai bungeni Dodoma.
Aliongeza: “Alipata tabu sana, lakini kwa sababu ni daktari pia amekuwa ni daktari wangu muda wote ndio maana mnaniona hapa vile nilivyo. Hakika wewe ni mke mwema… asante sana kwa kunipa raha, nakushukuru maana hata suti ya leo umeninunulia wewe nakushukuru sana”.
Ndugai aliwahi kusema bungeni kuwa katika maisha yake hakuwahi kuota, kuwaza au kufikiri kuwa angekuwa mwanasiasa au kuwa mbunge na Spika wa Bunge.
“Ni Mungu tu, Mungu wa ajabu ambaye katika uumbaji wake hutujua na wakati mwingi hutupangia safari kadri anavyoona ni vema,” alisema.
Ndugai aliwaeleza wabunge wa Bunge la 11 kuwa huwezi kuwa Spika wa Bunge na ukafanikiwa kama huungwi mkono na rais.
Alisema alizaliwa na kukulia Kongwa katika Kijiji cha Laikala kwenye eneo lenye nyanda kame lakini nyanda bora kwa malisho ya mifugo.
“Kutoka kijijini kwetu hadi shuleni ilikuwa kilometa nane kwa hiyo tulikuwa tunasoma siku tano kwa wiki Jumatatu hadi Ijumaa, nilikuwa nikitembea kilometa nane kwenda na kilometa nane kurudi nyumbani, kilometa 16 kwa siku siku moja. 16 mara siku tano kilometa 80,” alisema Ndugai.
Aliongeza: “Nimekulia maisha ya shida, dhiki na miaka mingine tukiwa na janga na njaa mkoani Dodoma, nilipitia maisha hayo. Nikiwa mdogo nililala kwenye kitanda cha kamba, nililalia ngozi ya ng’ombe na kwenye nyumba ya tembe na nilichunga sana ng’ombe”.
Ndugai alisema alisoma katika Shule ya Msingi Sagara wilayani Kongwa wakati anasoma Chuo cha Wanyamapori Mweka mkoani Kilimanjaro alikuwa miongoni mwa wanafunzi masikini sana na kuna wakati muda wa likizo hakuwa na nauli ya kutoka Moshi kwenda nyumbani Dodoma.
Alisema kuna wakati likizo ikifika alikuwa haendi kwao na alikuwa akijificha kukwepa kuulizwa na wenzake kwa nini alikuwa haendi nyumbani kwao.
“Nyumbani mimi nilikuwa mtoto wa pekee wa mama yangu, ‘how I missed my mother’ (nimemkumbuka mama yangu),” alisema Ndugai.
I am making a good salary from home $4580-$5240/week , which is amazing under a year ago I was jobless in a horrible economy. I thank God every day I was blessed with these instructions and now its my duty to pay it forward and share it with Everyone,
Here is I started_______ http://Www.EarnApp1.Com
***[JOIN US]***$26,000 or even more is very simple and easy to earns while staying and working online. Start receiving paychecks every month simply by doing work online. I recently received $27493 in my bank of my last month’s working. I just gave this job 2 hours maximum from my day. Simple and easy home based job.GOOD LUCK.:)HERE ====)> https://Www.Workapp1.Com