ATO wataka ushirikiano mageuzi ya kilimo 2050

DODOMA: Katika Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayoendelea Nzuguni, Dodoma, Ofisi ya Mageuzi ya Kilimo (ATO) imewasihi wadau wote wa sekta ya kilimo kushirikiana kikamilifu na ofisi hiyo ili kufanikisha utekelezaji wa dira ya kitaifa ya mageuzi ya kilimo.

Akizungumza kwa niaba ya ATO, Jeremiah Temu amesema dira hiyo ni matokeo ya ushirikiano mpana wa wadau mbalimbali na inalenga kulifanya kilimo kuwa mhimili wa uchumi wa kati na ustawi wa jamii.

“Kilimo kinaajiri zaidi ya asilimia 65 ya Watanzania, hivyo mageuzi ya sekta hii ni kichocheo kikuu cha maendeleo ya taifa. Tunatoa wito kwa taasisi, mashirika na sekta binafsi kuungana nasi katika safari hii,” alisema Temu.

Ujumbe huo umesisitiza umuhimu wa ushirikiano, ubunifu na uwekezaji wa pamoja katika kukuza tija na thamani ya kilimo nchini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button