Shirika laendelea kuimarisha uwezo wa wakulima

SHIRIKA la Heifer International Tanzania limeanza kutekeleza vipaumbele vya wakulima kwa kutumia mafunzo kutoka mashinani na mapendekezo yanayoongozwa na wakulima ili kukabiliana na changamoto kubwa zinazohusu ustahimilivu wa mabadiliko ya tabianchi na upotevu wa mazao baada ya mavuno.

Ndisha Joseph, Mshauri wa Ubora wa Maziwa, ameeleza kuwa Heifer inaendelea kuimarisha uwezo wa wakulima hasa katika ukusanyaji bora wa maziwa, upatikanaji wa vifaa vya kuhifadhi maziwa, kuanzisha na kuhifadhi malisho kwa ubora, na kuendeleza kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabianchi kwa lengo la kuongeza uzalishaji endelevu kwa wakulima wadogo.

Hatua hizi zinaonesha dhamira ya Heifer ya kushirikiana na wakulima katika kutafuta suluhisho la pamoja ili kuhakikisha maendeleo ya kilimo endelevu nchini Tanzania.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button