Rwanda yapinga tuhuma za kuisaidia M23

RWANDA : SERIKALI ya Rwanda imetupilia mbali tuhuma za Umoja wa Mataifa kwamba jeshi lake limekuwa likiunga mkono waasi wa M23 wanaopigana Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kuhusika katika mauaji ya mamia ya raia.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda imesema madai hayo yanaweza kudhoofisha juhudi zinazoendelea za kidiplomasia na mazungumzo ya amani ili kutatua mzozo huo. SOMA: Rwanda, DRC waanza kutekeleza makubaliano ya amani

Mwezi Agosti, Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk, alieleza kusikitishwa na mauaji ya raia 319 yaliyotekelezwa na M23 mwezi Julai, licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano.

M23, ambayo ilianza upya mashambulizi mwaka 2021 ikisaidiwa na Rwanda, imeteka maeneo kadhaa mashariki mwa DRC  na kusababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu katika eneo hilo lenye utajiri wa madini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button