Waandishi watakiwa kuandika habari za Dira 2050

WAANDISHI wa Habari wametakiwa kufanya uchambuzi na kuandika habari zinazohusu Dira ya Taifa 2050 iliyozinduliwa Julai,2025 ili kuhakikisha kila mwananchi anaelewa na kuwajibika kutekeleza .

Akizugumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo ya waandishi wa habari yaliyoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu(UNFPA) kwa kushirikiana na Tume ya Mipango, Melissa McNeil-Barrett amesema waandishi wa habari wanauwezo mkubwa wa  kuunda simulizi, kukuza sauti za wananchi, na kuweka jamii kwenye taarifa sahihi hivyo ni muhimu katika kubadilisha dira kuwa hai kwa wananchi.

“Pia mnaweza kutasaidia katika kuhakikisha uwajibikaji ili Dira ya 2050 iwe sio tu mfumo wa kitaifa, bali uhalisia wa pamoja wa kila mmoja. Mjadala huu unatupatia nafasi ya:

kuzidisha uelewa juu ya malengo ya Dira na ramani ya utekelezaji wake na mtajifunza  namna vyombo vya habari vinaweza kushirikisha wananchi kwa ubunifu kupitia majukwaa ya jadi na ya kidigitali,”amefafanua.

Aidha amesema pia mafunzo hay ohayo yatakuza ushirikiano kati ya serikali, washirika wa maendeleo, na vyombo vya habari ili kuhakikisha uelewa wa umma unaendelea kwa uthabiti na kutambua mchango wa wadau.Amesema wanapaswa ufafanua lugha tata ya sera na kuigeuza kuwa hadithi rahisi na zenye msukumo kwa Watanzania wote na kuonesha fursa zinazotolewa na TDV 2050 kwa jamii na hususan vijana.

“Kutushikilia kuwajibika kwa hatua tulizopiga huku mkisherehekea mafanikio njiani na kutumia majukwaa yenu kuhamasisha kila raia kuona nafasi yake katika utekelezaji na ufanikishaji wa malengo ya Dira,”amebainisha.

Ameongeza “Vyombo vya habari vitahamasisha ushiriki wa raia, na kuhakikisha kwamba kila Mtanzania kutoka jiji kubwa hadi kijiji cha mbali zaidi kutoka Kigoma hadi Zanzibar anaelewa na anajihisi mmiliki wa Dira hii.

Kwa upande wake Naibu katibu mtendaji -mipango ya Taifa-Tume ya Taifa ya mipango, Mursali Milanzi amesema kuandaa dira ni jambo moja na utekelezaji ni jambo lingine na kuwataka waandishi wanaweza kufikisha habari kwa wananchi na wadau wengine ili kuandaa wananchi katika utekelezaji wa dira.

“Utekelezaji huu wa dira utaanza rasmi mwaka wa fedha wa 2026/2027 kabla hatujafika huko ni vizuri kuwaandaa wadau mbalimbali kuelekea kwenye utekelezaji wa dira mpya.

Amesema wamewajenge waandishi wa habari kuhusu ni maudhui ya dira kuangalia ina misingi,malengo na shabaha kufikia 2050 .

“Kuna nguzo za dira kuna maeneo matatu kama uchumi,maendeleo ya watu na masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi,tumejadili namna gani mambo mbalimbali yanachoche utekelezaji wa dira pia tumezungumza namna serikali imeweka mifumo ya utekelezaji na ufuatiliaji ,mifumo ya usimamizi na mifumo ya uwajibikaji itasimamiwa na tume ya mipango,”amesisitiza Milanzi.

Aidha amesema wataendelea kushirikiana na wanahabari kutoa elimu ili kila mwananchi aweze kutoa mchango wake.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button