Vijana wapewa mbinu kujikwamua kiuchumi

MWENYEKITI wa Bodi ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Profesa Faustine Kamuzora amewashauri vijana ambao ni kundi kubwa na wenye nguvu ya kufanya kazi wawekeze kwenye mfuko huo ili wapate mtaji wa kujinyanyua kibiashara na kiuchumi katika maisha yao.
Profesa Kamuzora amesema hayo leo wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwenye kufungua kituo cha uwekezaji UTT AMIS huku akieleza wakiwekeza takribani miaka mitatu watakuwa wamekuza mitaji yao na kuondokana na wimbi la umaskini huku ikiendeleza dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 hadi 2050.
Profesa Kamuzora amesema vijana hawana budi kuwekeza kwani watu wengi wamekuwa masikini kwa kukosa elimu ya fedha hivyo wanapaswa wajibidishe na kuwekeza ili waweze kufaidika na kusaidia ndugu zao.

“Mnaweza kuweka fedha kidogo kidogo hasa vijana mtaweza kunufaika kwani shughuli mnazofanya za uchimbaji wa madini ,biashara na kilimo ni fursa kwenu kuwekeza sasa”amesema Profesa Kamuzora.
Mkurugenzi Mtendaji wa Uwekezaji UTT AMIS Simon Migangala amesema walianzs mwaka 2005 na asset ya shilingi bilioni moja na sass ni miaka 20 wameenda wakikuwa na kufikia asset ya shilingi bilioni 20 ambapo kila mwaka asset ilikuwa bilioni moja moja huku akieleza sababu za kukua kwao ni kujiamini na kuwepo uaminifu.
“Tunipongeza serikali kwa kuendelea kutuwezesha mazingira mazuri ya uwekezaji na kuwa bora kazi iliyobaki ni kuhudumia wananchi kuhakikisha wanawekeza na kupata faida kwa wakazi wa Kahama na Mikoa ya jirani,”alisema Migangala.
Migangala amesema sehemu kubwa huduma inapatikana zaidi kwenye mitandao na zinaendelea kuboreshwa kupitia tecknolojia na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu imeonekana kukuza uwekezaji nchini.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Frank Nkinda amesema tathimni iliyofanyika na kufungua kituo hiki imethihirisha kupanua wigo na kuwawezesha wananchi kupata elimu ya fedha na kuweka akiba.
Nkinda amewapongeza kwa kiasi cha rasilimali walichowekeza Sh trilioni 3.5 kwa wawekezaji 500,000 hivyo matumaini yaliyopo kwa ujio huo ni kuongeza ukuaji wa kiuchumi kwa wananchi wa wilaya hii.

“Serikali ipo sambamba na taasisi za kifedha kwa mujibu wa kisera itachochea na kuleta hamasa kwa wananchi wa mjini na vijijini ninawaomba kwenye mkutano na wachimbaji wadogo muwepo mtoe elimu hii waweze kuwekeza,”amesema Nkinda.
Baadhi ya wananchi walio hudhuria ufunguzi huo Herieth John na Daud James wamesema uwekezaji huo ni mzuri utawafanya kuinuka zaidi katika biashara zao na kusomesha watoto.



