TTCL yajizatiti vijijini changamoto ya mawasiliano

ARUSHA: SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania(TTCL) limejikita zaidi katika kupeleka huduma za mawasiliano nchi nzima haswa maeneo ya vijijini ambayo yanachangamoto ya mawasiliano kupitia mkongo wa taifa katika kufikia uchumi wa kigitali.
Akizungumzana wanahabari jijini Arusha kwenye kikao kazi cha 3 cha wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma (CEOs Forum 2025),Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Moremi Marwa amesema uchumi wa kidigitali utafikiwa kwa wananchi kupata mawasiliano mazuri katika maeneo mbalimbali kupitia shirika hilo

Amesema katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia wananchi serikali kupitia shirika hilo imewekeza kwenye minara ya mawasiliano 1,400 na hadi sasa TTCL imeshasambaza huduma zake katika minara 626 na hadi kufikia mwakani minara mingine 850 itajengwa maeneo mbalimbali nchini haswa vijijini ambayo yanachangamoto ya mawasiliano
“Minara hiyo inaunganishwa na mkongo wa Taifa katika kuhakikisha uchumi wa kigitali unafikiwa kwa kupata mawasiliano bora kwa wananchi na mwaka 2026/27 tutakamilisha usimikaji wa minara mingine 850”

Amesisitiza shirika hilo katika kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 limejikita zaidi kuboresha huduma zake kwa jamii na kuwezesha TTCL kuwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kutokana uwepo wa miundombinu bora ya mawasiliano yenye uwezo wa kufanikisha ukuaji wa uchumi wa kidjitali.



