Kumekucha kampeni za Uchaguzi Mkuu

WAGOMBEA urais 17, ubunge na udiwani leo wanatarajiwa kuanza kampeni kuomba wananchi wawapigie kura katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, mwaka huu.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ilifanya uteuzi wa wagombea hao Agosti 27 wakiwemo 17 wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na INEC kampeni za uchaguzi zinaanza leo hadi Oktoba 28, mwaka huu kwa Tanzania Bara.
INEC imetangaza kampeni za uchaguzi kwa Tanzania Zanzibar zinaanza leo hadi Oktoba 27 mwaka huu ili kupisha kura ya mapema na Oktoba 29, mwaka huu itakuwa siku ya kupiga kura nchi nzima.
SOMA: Wagombea zingatieni ratiba za kampeni
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (INEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenan Kihongosi amesema kampeni za CCM katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu zitakuwa za kihistoria.
Kihongosi amesema hayo wakati akikagua maandalizi ya uzinduzi wa kampeni za chama hicho unaofanyika leo katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Dar es Salaam.
Samia kufungua dimba leo Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza maelfu ya wanachama kwenye uzinduzi huo.
Januari 19, mwaka huu wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM walimpitisha Samia agombee urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
“Ni kampeni za aina yake, ni kampeni ambazo hazijawahi kuonekana tangu kuanza kwa siasa za nchi hii, mtaona mambo makubwa na mambo mazuri sana, mambo ya CCM nadhani mnayafahamu hakuna jambo dogo ndani ya CCM,” alisema Kihongosi.
Aliongeza: “Kampeni za CCM zitakuwa za kistaarabu ambazo zimebeba misingi ya amani, kulinda utu na amani kwa maana kwamba tutaenda kufanya kampeni kwa kutumia hoja hakutakuwa matusi hatutatweza wala kudhalilisha utu wa mtu mwingine”.
Kihongosi alisema katika uchaguzi wa mwaka huu CCM imekuja na Ilani bora iliyobeba matumaini ya Watanzania katika sekta zote zinazogusa maisha yao na imeweka wagombea wenye uwezo na uzoefu wa kutosha wa uongozi.
Alisema CCM itatumia uzinduzi huo kunadi wagombea ubunge wa majimbo 12 ya Mkoa wa Dar es Salaam na wagombea udiwani.
Alisema baada ya uzinduzi unaofanyika leo kampeni za CCM zitahamia Mkoa wa Morogoro, Dodoma na baadaye chama kitatangaza ratiba ya mikoa inayofuata.
NLD
Mgombea wa urais wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo alisema chama hicho kinatarajia kuzindua kampeni Septemba 4, mwaka huu katika viwanja vya kituo cha mabasi cha Pangani, Tanga.
AAFP
Mgombea urais wa AAFP, Kunje Ngombale Mwiru alilieleza HabariLEO wanatarajia kuzindua kampeni zao Kilosa, Kisaki au Matombo mkoani Morogoro.
“Tumechagua maeneo hayo kwa sababu sisi ni chama cha wakulima kwa hiyo tumeamua kampeni zetu kuzindulia katika maeneo yenye wakulima,” alisema Kunje.
Makini
Mgombea wa urais kupitia Chama cha Makini, Coaster Kibonde alilieleza HabariLEO kampeni za chama hicho
zitazinduliwa Septemba 2 mwaka huu katika viwanja vya Bakhresa, Manzese mkoani Dar es Salaam.
UMD
Mgombea urais wa Union for Multiparty Democracy (UMD), Mwajuma Mirambo alisema kampeni za chama hicho zitazinduliwa Muheza, Tanga.
ADA-TADEA
Mgombea urais wa ADA–TADEA, Georges Bussungu alisema chama hicho kinatarajia kuzindua kampeni Septemba 14, mwaka huu katika Viwanja vya Zakhiem Mbagala, Dar es Salaam.
SAU
Naye mgombea urais kupitia Sauti ya Umma (SAU), Majalio Kyara alisema chama hicho kinatarajia kuzindua kampeni na kaulimbiu ya chama hicho jijini Dodoma mwanzoni wa mwezi ujao.
CCK
Kwa upande wake mgombea urais wa CCK, David Mwaijojele alilieleza HabariLEO kampeni za chama hicho zitazinduliwa Kijichi, Dar es Salaam Agosti 30 au 31, mwaka huu.
CHAUMMA
Mgombea urais wa CHAUMMA, Salum Mwalimu alisema taarifa juu ya ratiba za kampeni zitatolewa baadaye,
CUF Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kinatarajia kuzindua kampeni Agosti 31 au Septemba Mosi, mwaka huu katika uwanja wa Furahisha wilayani Ilemela, Mwanza.
UPDP
Mwenyekiti wa UPDP, Twalib Kageze alisema wamepanga kuzindua kampeni zao Septemba 5, mwaka huu kwenye uwanja wa Nyamagana, Mwanza.
NCCR Mageuzi
Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Eveline Munisi alisema watazindua kampeni Septemba 6, mwaka huu katika Jimbo la Buhigwe, Kigoma.
Imeandikwa na Eva Sindika, Shakila Mtambo na Ally Ruambo.
I make $88 an hour to work part time on a laptop. I never thought it was possible but my closest friend easily made $18,000 in 3 weeks with this top offer and she delighted me to join. .Visit the following article for new information on how to access…….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
I am pleased that I noticed this site, precisely the right information that I was searching for! .