Tanfoam Marathon kuvuta washiriki 1300

MSIMU wa pili wa mbio za riadha za Tanfoam umepangwa kufanyika Desemba 7 mwaka huu jijini Arusha huku ukirajiwa kuvuta washiriki mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Zaidi ya washiriki 1300 wanatarajiwa kushiriki mbio hizo za kilometa 5,kilometa 10 ,kilometa 21 na mbio ndefu za kilometa 42 ambazo zimejumuishwa katika msimu huu wa pili wa mbio hizo.

Akizungumza jijini hapa Mwenyekiti wa Mbio za Tanfoam Marathon Glorious Temu amesema ni tukio la kipekee na lenye uzito mkubwa katika kuendeleza sekta ya michezo nchini ambapo msimu huo wa pili utafanyika katika viwanja vya General Tyre jijini hapa.

“Michezo ni zaidi ya burudani katika jamii na kichocheo cha afya bora na kupitia Tanfoam Marathon tunadumisha dhana kuwa Taifa lenye afya ni lina nguvu na mshikamano na msimu huu tumepania kuandaa mbio za kipekee zaidi huku tukiwashirikisha wakimbiaji wa ndani na kimataifa na si kuinua vipaji pekee bali kuitangaza Arusha na Tanzania kama kitovu cha mendeleo,” amesema Temu.

Ameushukuru uongozi wa Tanfoam kwa na wadau wote kwa kuwaunga mkono na kuongeza kuwa wana Arusha wajitokeze na wafike kushiriki huku akibainisha kuwa zawadi kwa walioshiriki mwaka jana walipata pesa na bidhaa zingine hivyo mwaka huu zitakuwa zaidi.

Naye, Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania Rogath Steven amesema Tanfoam Marathon ni moja mbio kubwa sana hapa nchini ambayo imekuwa ikiandaliwa kwa kufuata taratibu zilizowekwa na shirikisho la Riadha Tanzania (RT).

“Natoa wito kwa waandaaji wote kuzingatia mbio za watoto na zitakuwa lazima ziwepo kwa kila mwandaaji awahusishe ili tuweze kutengeneza kizaji kujacho ambacho kitawarithi wanariadha wetu waliopo na sisi tutatoa ushirikiano na tutaweka taratibu hizo kuanzia mwakani,” amesema Steven.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button