Usomaji endelevu waja kukuza umahiri enzi ya kidijitali

MOROGORO: SEPTEMBA 8 hadi 9 kila mwaka Tanzania inaungana na mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Kusoma Duniani inayolenga kufuta ujinga na kuendeleza dhana ya usomaji endelevu.
Maadhimisho haya yaliasisiwa mwaka 1965 katika mkutano wa dunia wa mawaziri wa elimu waliokutana Tehran , Iran. Moja ya mapendekezo ya Tehran,ni kuanzishwa kwa siku ya usomaji duniani,ili kuendeleza dhana ya usomaji endelevu.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),linasema kumekuwa na hatua kubwa katika miongo kadhaa iliyopita.
Maadhimisho ya usomaji duniani kwa mkoa wa Morogoro yanafanyika eneo la maktaba ya mkoa na kilele chake ni Septamba 9, ambapo yanayarajiwa kufungwa na mkuu wa mkoa huo , Adam Malima.

Kauli mbinu ya maadhimisho ya Mwaka huu 2025 ni :” Kukuza Umahiri katika Enzi ya Kidijitali”.



