Wananchi 5,700 wapata uhakika wa maji safi Chato

WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Chato mkoani Geita imekamilisha mradi wa maji katika kijiji cha Minkoto na kuwezesha uhakika wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wapato 5,724.

Meneja wa Ruwasa wilayani Chato, Mhandisi Avitus Exavery ametoa taarifa ya mradi huo Septemba 07, 2025 mbele ya viongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2025 katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la uzinduzi rasmi wa mradi huo.

Mhandisi Avitus amesema mradi umegharimu kiasi cha sh milioni 249 kutoka vyanzo tofauti zimelipwa na utekelezaji wa mradi ulianza Februarii 12, 2024 hadi Oktoba 30, 2024.

“Mradi ulihusisha ujenzi wa mtandao wa bomba umbali wa kilomita 12.189, ujenzi wa tenki la moja la ujazo wa lita 50,000 na ununuzu wa pampu na sola za umeme.

“Chanzo cha maji cha ni kisima kirefu cha mita 75 chenye uwezo wa kuzalisha lita 5,500 kwa saa ambapo mradi huu umelenga kutatua changamoto ya maji kwa wananchi wote wa kijiji cha Minkoto”, amesema.

Amesema katika kusogeza huduma kwa wananchi, Ruwasa imejenga 10 vya kuchotea maji, kusambaza mtandao wa bomba la maji mita 10,821 pamoja na kuwaunganishia maji wananchii binafsi kwenye makazi yao wapato 40.

Amesema hamasa inaendelea kushawishi watu wengine waweze kuunganishiwa na kuendeleza juhudi za kusaidia kupunguza magonjwa ya mlipuko kwa wananchi kutumia huduma ya maji safi na salama.

Mkuu wa Wilaya ya Chato, Louis Bura amesema mbali na wananchi wa kawaida kunufaika pia wanafunzi wa shule zinazozunguka eneo la mradi zitapata huduma ya maji safi na salama ya uhakika.

Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Mwaka 2025, Ismail Ali Ussi amesema malengo ya serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha inamtua mama ndoo kichwani hivo juhudi ziendelee kupanua zaidi mtandao wa maji.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button