Mwenge wazindua mabweni Kyaka sekondari

KAGERA: Mwenge wa Uhuru umezindua bweni la wasichana wa kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Kyaka iliyopo wilayani Missenyi mkoani Kagera.

Bweni hilo lenye vyumba viwili ambalo limegharimu Sh milioni 260 imeelezwa kuwa ni chachu kuwajengea uwezo wanafunzi wa kike wanaotarajiwa kujiunga na shule hiyo mwaka 2026/2027.

Akisoma taarifa ya mradi kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Ismail Ali Ussi, Mkuu wa Shule hiyo, Fadhir Nnko amesema fedha ya ujenzi wa mabweni hayo ilitoka Serikali Kuu ambapo mradi huo ulianza kutekelezwa Machi 15 ,2025 na kukamilika Agosti 20 mwaka huu kwa asilimia 100.

“Bweni hilo lina uwezo wa kulaza wanafunzi 160 wa kidato cha tano na sita kwa wakati mmoja ambao wanatarajiwa kudahiliwa mwaka ujao wa masomo kutoka maeneo mbalimbali ya nchini na itasaidia kuondoa adha za watoto wa kike kutembea umbali mrefu kuja shule na kuepukana na changamoto za kuwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia,” amesema Nnko.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Ismail Ali Ussi amesema serikali itaendelea kujenga miundo mbinu ya mabweni kwa wanafunzi bila kujali umbali wala mji au kjiji na kudai kuwa popote palipojengwa miundombinu bora ya elimu watoto wanasoma kwa adilifu, uzalendo na ukomavu wa hali ya juu.

“Rais Dk Samia Suluhu Hassan aliona ipo haja leo hii kuwa wapo wanafunzi ambao wanapokaribia kipindi cha mwaka wa masomo wanapata adha ya kutembea umbali mrefu kufata huduma hiyo na serikali imeona ipo haja ya kuhakikisha shule za kata zilizokidhi vigezo kuanzisha kidato cha tani na sita ili Kila mwanafunzi anayehitimu kidato cha nne mwenye ufahulu mzuri apate fursa ya kujiunga na kidato cha tanio,”amesema Ussi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Missenyi, kanali Hamis Mayamba wakati akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Sima amesema mwenge utakagua, utatembelea na kuweka mawe ya msingi Katika miradi saba yenye thamanj ya Sh bilioni 2.4

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button