Mfanyabiashara mlemavu apewa tabasamu Babati

MANYARA: Ramadhani Omar mkazi wa mtaa wa N’gwan’gwarai wilayani Babati mkoani Manyara ni kijana mwenye ulemavu wa viungo lakini ni mtu anaejishighulisha na biashara ya uuzaji wa mahindi ili aweze kulea familia yake.

Lakini Ramadhani anakutana na changamoto kwenye biashara yake kutokana na ulemavu wake anakuwa anaonewa na Watu anaowatuma kumletea mahindi ili aweze kuuza kwa wateja wake: “Mimi ni mfanyabiashara zamani nilikuwa nafuata mahindi mwenyewe porini kwa kutumia pikipiki lakini nikituma mtu kuna changamoto nyingi changamoto ya kwanza unaweza kuletewa mahindi mabovu hayana kiwango,”

“Changamoto ya pili unaweza kuletewa mzigo hauja jaa inabidi sasa nifate mwenyewe nakodisha pikipiki kuchukua mzigo nilete nyumbani ili niweze kuuza wakati mwingine unaita pikipiki anachelewa kufika na unakuta wateja ni wengi kwahiyo inakuwa ni changamoto kubwa sasa baada ya kupata pikipiki hii kwakweli nitaweza kufanya biashara Yangu vizuri na nitafanya kwa wakati Asante Mati Foundation kwa kunisaidia endeleeni kusaidia na wengine, “amesema Ramadhani.

Mama wa Ramadhani aitwaye, Asia Ramadan yeye analia na wale wanaokuwa chanzo cha kumrudisha nyuma kijana wake kwenye biashara yake “maisha ni magumu kwa sababu gani tangu alipoanza kuwa miguu ilipoanza kugoma akawa hana maisha yakutosha msaada wake ukawa mdogo sana na biashara zake izo anazozifanya mara nyingine biashara zake zinakufakufa msaada wake ni mdogo kimaisha halafu biashara yake ni mahindi inakufa kila mara kwa sababu watu wanakuja wanachukua halafu hawalipi kwa wakati sasa ikichukua muda hiyo biashara siitakua imesimama,”amesema Mama wa Ramadhani.

Baada ya kuhangaika kutafuta namna ya kuweza kukabiliana na changamoto zinazomkabili Ramadhani sasa anatabasamu baada ya wadau kutoka Mati foundation ambayo ipo chini ya Mati Super Brand LTD wakiongozwa na meneja wa Mati Foundation Izack Piganio kuona changamoto yake na kuweza kuitatua na kumpatia pikipiki yenye magurudumu matatu ambayo itaweza kumsaidi kuweza kufata mwenyewe mahindi Huko shambani na maeneo yote yanapopatikana na kuuza kwa wakati

“Kwakipindi hiki tumekuwa na program ya kurudisha tabasamu kwa wananchi kupitia pikipiki hizi za walemavu hasa kwa wana Manyara na mikoa mingine inayotusapoti sisi kama Mati Super Brand kwa siku ya leo tumeanza na Manyara walitupokea vizuri kama mnavyofahamu ndugu waandishi kampuni yetu ipo mkoa wa Manyara na sisi tunarudisha kwa jamii kama shukrani,”amesema Piganio

Pia Mkurugenzi wa Kampuni ya vinywaji changamshi Mati super brand LTD David Mulokozi amesema ameamua kutoa pikipiki hizo ili kuwasapoti walemavu wanaojishughulisha ” Tumezingatia kuangalia wale ndugu zetu wenyeulemavu ambao wanaojishughulisha na majukumu yao ya kila siku kwahiyo tumeona tuwapatie pikipiki hizi za umeme,”amesema Mulokozi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button