Waandishi waandikeni wagombea udiwani

DAR-ES-SALAAM : MJUMBE wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Dk. Rose Reuben amewashauri waandishi wa habari kuhakikisha wanaripoti habari za wagombea wa udiwani, ambao mara nyingi husaahauliwa katika taarifa za mikutano ya kampeni.

Akizungumza katika mkutano wa kuwakaribisha wanachama wapya wa TAMWA uliofanyika kwa njia ya mtandao wa Zoom, Dk. Rose alisema waandishi wengi wameegemea kuripoti wagombea wa urais na ubunge huku wagombea wa udiwani wakiwa kando.

“Wagombea wa udiwani wana haki sawa na wagombea wa urais na ubunge ya kutangazwa na kuzungumzia sera za vyama vyao,” alisema Dk. Rose. SOMA: TCRA yatahadharisha uchochezi habari za uchaguzi

Dk. Rose alisisitiza kuwa waandishi wanapaswa kutoa taarifa za wagombea wote bila ubaguzi wowote. Aidha, aliwashauri waandishi kuendelea kufuata sheria za uchaguzi na kuhakikisha kila mwandishi anayeripoti habari za uchaguzi ana kitambulisho cha Ithibati, hatua inayolenga kupunguza matatizo ya kisheria.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button