“Iungeni mkono CCM”

TANGA: Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Rajab Abdulrahaman amesema kuwa maendeleo ni mchakato hivyo wananchi waendele kukiunga mkono chama hicho kwani kinaendelea kuleta maendeleo kupitia utekelezaji wa ilani yake
Kauli hiyo ameitoa wakati wa ufunguzi wa kampeni za ubunge katika Jimbo la Korogwe Vijijini ambapo amesema kuwa Ilani ya uchaguzi imetekelezwa kwa mafanikio makubwa hivyo wananchi hawana sababu ya kutokiunga mkono chama tawala.
Amesema kutokana na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kwa kiwango kikubwa, hawana sababu ya kutokiunga mkono chama hicho. “Mkoa wa Tanga chama kimefanya makubwa kama kwenye sekta ya elimu awamu ya sita imeweza kujenga shule mpya za msingi 95 pamoja na Sekondari 72 huku wakiteleza sera ya elimu,”amesema.
Kwa upande wake mgombea ubunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Timotheo Mnzava amewataka wananchi kuendelea kumuunga mkono ili aweze kuendelea kuwaletea maendeleo kwenye jimbo hilo.
“Tumeweza kufanya mengi kwenye sekta za elimu,afya ,miundombinu ya barabara hivyo naomba endeleeni kuniamini ili niweze kuendelea kuwaletea maendeleo,”amesema Mnzava.



