Dk Nchimbi awasili Tanga mwendelezo wa kampeni

TANGA: Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk Emmanuel Nchimbi amewasili mkoani Tanga kuendelea na kampeni ya kusaka kura za ugombea wa urais, wabunge na madiwani.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajab Abdulrahaman amesema kuwa mgombea huyo atafanya mikutano ya hadhara sambamba na kuongea na wanachama wa chama hicho .
Amesema kuwa Dk Nchimbi anatajiwa kutembelea wilaya za Bumbuli, Korogwe, Handeni, Kilindi, Muheza na Mkinga ambapo atatumia fursa hiyo kunadi Ilani ya chama hicho .
- “Niwaombe wanatanga kuweza kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano hiyo ya kampeni kwani Tanga mpaka sasa hali ya kisiasa ni nzuri hakuna malalamiko vyama vyote vinafanya kampeni kwa usawa,” amesema mwenyekiti huyo.



