Viongozi wahimizwa kutoa elimu nishati safi

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Ismail Ali Ussi amewataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri zote za Mkoa wa Kagera  kuwahamasisha wananchi kutumia nishati safi ili kuepukana na athari za kiafya zitokanazo na nishati chafu.

Ametoa wito huo akiwa wilayani Biharamulo ambapo amesema viongozi hao wa napaswa kwenda sambamba na wananchi juu ya elimu ya matumizi ya nishati safi na kudai Rais Dk Samia Suluhu Hassan  ndio kinara wa nishati safi  na kampeni ya matumizi ya nishati inapaswa kutekelezwa na kila mtu.

Akizindua mfumo wa matumizi ya nishati safi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa Shule ya Msingi Biharamulo, amesema taasisi zinazo hudumia watu zaidi ya 100 zinapaswa kujiunga na mfumo wa matumizi ya nishati safi ili kuokoa mazingira na kuendana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Katika Mkoa wa Kagera kupitia mbio za Mwenge wa Uhuru  mkoani Kagera kiongozi huyo amegawa mitungi ya gesi kwa wajasiliamali wadogo mama lishe na baba lishe na taasisi za umma yapatayo 1054 ili kuendeleza hamasa ya matumizi ya nishati safi

“Kufikia 2030 tunapaswa kuwa na asilimia 80 ya wanaotumia nishati safi niombe kampeni ya maswala ya nishati safi iendelee na hata kupitia mikutano yetu ngazi ya halmashauri hadi vijiji iwe ajenda ya Kudumu,”amesema Ussi.

Benson Mwamelo ni Ofisa Misitu Wilaya ya Biharamulo akitoa taarifa  kwa kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Ismail Ali Ussi juu ya mradi wa Nishati safi katika Shule ya Msingi Biharamulo (A) yenye kitengo cha elimu maalum  amesema wilaya hiyo wanaendelea kuwasaidia wananchi na kuhakikisha   wanatumia nishati safi ambapo ni njia moja wapo ya kukabiliana na matumizi ya mkaa na kuni.

Amesema halmashauri hiyo imetoa zaidi ya  Sh milioni 9 kutokana na mapato ya ndani ambapo kwa ajili.

ya kufunga majiko mawili ya kisasa sufuria zinazotumika kwenye kupikia mitungi minne ya gesi na kufunga miundombinu yake ambayo ni kuunga mkono kampeni ya serikali ya matumizi ya nishati safi kwa vitendo.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Advera Bulimba amesema Mwenge wa Uhuru umezindua, kukagua na kuweka mawe ya msingi Katika Miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya Sh bilioni 2  ikiwemo elimu afya, barabara, maji na nishati safi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button