Dk Mussa awafunda viongozi vyama vya ushirika Morogoro

MOROGORO: VIONGOZI wa Bodi za Vyama Vikuu vya Ushirika Mkoa wa Morogoro wametakiwa kufuata sheria , kanuni na taratibu katika kuingia mikataba ili kuepuka kuviletea hasara ya mali na fedha vyama hivyo.

Katibu Tawala wa mkoa huo, Dk Mussa Ali Mussa amesema hayo akifungua mafunzo ya siku tatu kwa viongozi vyama vikuu vya ushirika vilivyopo mkoani humo.

“Katika suala la mikataba ,lazima viongozi wa bodi fuateni sheria wakati wa kuingia mikataba na shirikisheni wanasheria kuepuka uviingiza vyama kwenye kupata hasara na matizo,” amesema Dk Mussa.

Katibu Tawala wa Mkoa huyo amewataka viongozi wa bodi ya vyama vikuu hivyo kuzingatia misingi ya maadili kwenye utendaji kazi zao pamoja na kujiepusha na vitendo vya rushwa na upendeleo.

Pia amewataka viongozi hao kuajiri watu wenye sifa zilizoainishwa kulingana na nafasi zinazohitajika badala ya kuajiri wasiona sifa,kitendo ambacho watashindwa kusimamia masuala ya ushirika ikiwa na kujielekeza kwenye matumizi ya mifumo ya kidijitali na akili mnemba.

Katibu Tawala wa mkoa huyo amewaasa viongozi wa bodi ya vyama hivyo wasivigeuze kutumika katika masuala ya kisiasa.

“Chama kikuu cha ushirika kisiwe na mlengo wa kisiasa bali wanachama wake wanaweza kuwa na itikadi ya vyama tofauti lengo ni kuepuka kuathiri misingi ya umoja,” amesema Dk Mussa.

Mbali na hayo amewataka waratibu wa vyama hivyo mkoani humo kusimamia vema ukaguzi wa hesabu mara kwa mara ndani ya vyama vya ushirika na kuviimarisha vile inavyohitajika.

Amesema, uwepo wa ukaguzi hesabu wa mara kwa mara utasaidia upatikanaji wa hati safi na hivyo kuimarisha utunzaji wa hesabu na uhifadhi mzuri wa nyaraka katika vyama hivyo.

Naye Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Morogoro,Cesilia Sostenes amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo viongozi wa bodi hizo katika maeneo mbalimbali yamewashirikisha wenyeviti wa bodi ,watendaji wa Bodi ambao ni Mameneja na wahasibu.

Cesilia amesema mkoa huo una vyama vikuu vitatu ambavyo ni Ukiku , Kicu na Mofacu pamoja kingine cha Magole Joint ambacho kinajihusisha na kilimo cha miwa .

Ametajaeneo lingine katika kuujua ushirika ,majukumu ya wajumbe wa bodi , elimu ya manunuzi , mifumo ya kidijitali , sheria za mikataba, masuala ya ukaguzi na uandishi wa vitabu vya hesabu ili kundoa hati chafu

Kwa upande wake Mkaguzi wa Vyama vya Ushirika mkoa huo, Damian Mashauri amesema matumizi ya mifuno ya kiteknolojia inasadia mambo mengi ikiwemo kutunza kumbukumbu sahihi na kurahisisha upatikanaji wa taarifa pale zinapohitajika na mazoezi ya ukaguzi

“Tayari kuna vyama vya ushirika vipo kwenye mifuno ya kidijitali na kimsingi imewasaidia baadhi ya vyama kuhakikisha taarifa zao zipo na pia kutunza kumbukumbu za muda mrefu na matumizi sahihi ya kihasibu,”amesema Mashauri.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I get paid over 220 Bucks per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. the potential with this is endless…,

    COPY HERE➤➤ https://work99.site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button