Mwalunenge: Nipeni ubunge nibadilishe Mbeya

MBEYA : MGOMBEA wa nafasi ya Ubunge jimbo la Mbeya Mjini,Patrick Mwalunenge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) amewataka wakazi jijini Mbeya kumpa ubunge akisema lengo lake kupitia CCM kulibadilisha hilo kimaendeleo
Mwalunenge ametoa ahadi hiyo katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Soko Dogo Mtaa wa Isanga Kati, Kata ya Isanga ikiwa ni muendelezo wa kazi ya kujinadi kwa wananchi kuelekea uchaguzi Mkuu ujao. SOMA: “CCM itashiriki uchaguzi na vyama vingine”
Amewataka wakazi wa jimbo hilo kutambua kuwa ahadi zinazotolewa na CCM wakati huu wa kampeni ni Mkataba kati ya wagombea na wananchi hivyo iwapo atapewa ridhaa ya kuwa mbunge atahakikisha zinatekelezwa.
Miongoni mwa ahadi alizotoa kwa wakazi wa Kata ya Isanga ni pamoja na kuhakikisha barabara zote zinapitika wakati wote kwa kusimamia serikali kuongeza mtandao wa barabara za lami na pia kuimarisha mitaro ya maji kwa barabara za kiwango cha changarawe ili ziwe bora.



