Dk Samia kufanya kampeni Sept 23 Mtwara

MTWARA: RAIS wa Tanzania na mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan, anatarajia kufanya kampeni ya Uchaguzi Mkuu kuanzia Septemba 23-26 mkoani Mtwara.

Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Mtwara, Juma Namkoveka ametoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari leo Septamba 20, 2025.

Namkoveka amesema Rais atawasili Mtwara asubuhi akitoa Mkoa wa Ruvuma na atapokelewa katika Wilaya ya Nanyumbu.

“Katika ziara hiyo, Raisi Dk Samia Suluhu Hassan atakutana na wananchi kupitia mikutano na ya kampeni kwa ajili ya kuwaeleza dira, sera na mikakati ya CCM kwa maendeleo ya taifa kupitia ilani ya Uchaguzi wa CCM ya mwaka 2025-2030,” amesema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button