“Nitaondoka michango isiyo na tija shuleni”

DAR ES SALAAM: MGOMBEA Udiwani Kata ya Zingiziwa kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Selemani Kaniki ameahidi kufuatilia kikamilifu na kuindoa kero ya michango isiyo na tija mashuleni.

Amesema ikiwa atachaguliwa kuongoza kata hiyo kwa miaka mitano ijayo ataanza na kero akisaidiana na mgombea ubunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa pamoja na Mgombea urais, Samia Suluhu Hassan.

Kaniki ameyasema hayo katuka mkutano wake wa 13 wa kampeni katika Kata ya Zingiziwa ambao umehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa chama pamoja na wananchi.

Akieleza hayo aliwataka walimu na wananchi kushirikiana naye pale atakapoingia madarakani kupanga mkakati mzuri utakaofaa ili kuwaepusha wananchi na kero wa michango isiyo na tija mashuleni.

Pia amewataka wazazi kuwa wahudhuriaji wazuri katika vikao mashuleni ili kuwa na maamuzi yatakayokuwa sahihi kwa kila mmoja ili kuepuka keri hiyo kwao na kwa wanafunzi.

“Hudhurieni vikao mashuleni ili tuondoe kero na masikitiko kama haya yanapokuja kutokea niwaahidi wanafunzi na mnaopata shida hiyo ambayo Rais Samia Suluhu Hassan alitoa elimu hii bure bila michango nitaenda kufuatilia kikamilifu,” amesema Kaniki.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button