MCP yadai kuibiwa kura uchaguzi Malawi

MALAWI : CHAMA Tawala cha Malawi, Malawi Congress Party (MCP), kinachounga mkono Rais Lazarus Chakwera, kimesema kina ushahidi wa wizi wa kura, huku matokeo ya awali yakionyesha kuwa kinashindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika wiki iliyopita.

Vitumbiko Mumba, mgombea mwenza wa Rais Chakwera, amesema baadhi ya watu walijaza karatasi bandia za kupigia kura katika masanduku ya kura. Aidha, amesema matokeo ya awali hayalingani na takwimu zilizotangazwa katika vituo vya kuhesabu na kujumlisha kura. SOMA: Mutharika aongoza matokeo ya awali urais

Hata hivyo, chama hicho hakijaonyesha ushahidi wowote wa tuhuma hizo hadharani. Mumba ameongeza kuwa MCP imetuma malalamiko yake kwa Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC), ambayo ina hadi Septemba 24 kutangaza matokeo rasmi ya urais.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button